Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na walemavu Mhe. Je nista Mhagama
……………………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-Maelezo
Vijana wameaswa kuacha kukaa
majumbani na kusubiri fursa za maendeleo ziwafate walipo na badala yake
watumie muda mwingi kujishughulisha kwa kufuata fursa zilipo ili
kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini.
Akizungumza hayo wakati wa
uzinduzi wa Kitabu cha taarifa ya utafiti wa Sauti za Vijana Tanzania
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na walemavu Mhe. Je nista
Mhagama amesema kuwa vijana wasikae majumbani na vijiweni kutegemea
Serikali iwapelekee fursa hizo.
“Vijana tusikae majumbani na
kushinda vijiweni tukitegemea kwamba tutawaletea fursa huko mlipo ,
mnatakiwa mtoke na mtumie muda wenu kufikiri jinsi ya kujikwamua na
tatizo la ukosefu wa ajira kwa kutumia fursa zitolewazo” alisema Mhe.
Mhagama.
Aidha Mhe. Jenista alisema kuwa
Serikali imeanza kutenga Shilingi Bilioni 15 kila bajeti kwa ajili ya
kukuza ujuzi na kujikwamua kiuchumi ili kuleta maendeleo kwa vijana na
taifa kwa ujumla.
Mbali na hayo Mhe. Mhagama
aliunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwamba
ni marufuku kwa kumbi za starehe na mahali popote kuuza kilevi aina ya
shisha kwani kinaharibu nguvu kazi ya vijana wa leo.
“Nasisitiza tena marufuku kwa
kumbi za starehe na mahali popote kuuza kilevi aina ya shisha kwani
inaharibu uwezo wa kufikiri kwa vijana na kushindwa kufanya kazi matokeo
yake uchumi wa nchi unazorota ,kwa yeyote atayekiuka maagizo haya hatua
kali zitachukuliwa juu yake.
Aidha Mhe. Jenista aliwataka
vijana kutumia vizuri fursa iliyotolewa na Serikali ya awamu ya tano kwa
kutoa Shilingi Milioni 50 kwa kila kijiji ili kuleta chachu ya
maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.
0 maoni:
Chapisha Maoni