Matukio ya ndege kupotea yanaonekana kuzidi kujitokeza baada ya muda mfupi ulipita kuripotiwa taarifa ya kupotea kwa ndege ya Jeshi la India (India Air Force) kupotea ikiwa na watu 29.
Ndege hiyo iliyo na namba AN-32 ilikuwa ikitokea Tambaram, Chennai na kuelekea kisiwa cha Port Bair&Nicobar kilichopo katika Ghuba ya Bengali na ilikuwa imekadiliwa kufika saa 11:30 asubuhi kwa saa za India lakini mawasiliano mara ya mwisho yalifanyika 8:45 asubuhi.
Tayari kikosi cha wanamaji cha jeshi la nchi hiyo kimepeleka meli kubwa kwa ajili ya kuitafuta ndege hiyo ambayo inaelezwa imepotea kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.