Jumatano, 27 Julai 2016

Wagonjwa 45,000 wa saratani hugundulika tanzania kila mwaka

UG1Mhe Ummy Mwalimu  akiwa na waziri wa afya (Uganda) Mhe .Sara Opendi na Mhe Omar Sey Waziri wa Afya wa  Gambia.
UG2Waziri wa afya Ummy Mwalimu akifuatilia mkutano huo
UG3.Picha ya pamoja ya wake wa marais na mawaziri wa afya wa afrika,waliohudhuria mkutano wa 10 wa kupambana na saratani ya shingo ya Kizazi,matiti na tezi dume (picha/habari na wizara ya afya)
……………………………………………………………………………………………………….
Na.Mwandishi wetu,Addis Ababa
Ugonjwa wa saratani nchini Tanzania  ni chanzo cha magonjwa na vifo,hivyo inakadiriwa Takribani wagonjwa wapya wa saratani 45,000 hugundulika kila mwaka.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika Mkutano wa 10 wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unaofanyika nchini hapa.
Waziri Ummy amesema kati ya wagonjwa hao asilimia 38  ni wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, asilimia 14  saratani ya ngozi, asilimia 10  saratani ya matiti na saratani ya tezi ni asilimia 4
Hatahivyo,takribani watu 35,000 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya Saratani.
Licha ya changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za kukabiliana na magonjwa hayo ikiwemo  uhaba wa Miundombinu ya kutolea huduma za afya, vifaa tiba, Uhaba wa Watumishi wa Afya, rasilimali fedha na gharama kubwa za dawa za matibabu ya saratani,Waziri Ummy amesema Serikali ya Tanzania  imepitisha Sera za Kitaifa na Miongozo mbalimbali ya Kupambana na Saratani, kutoe Elimu kwa jamii na watoa huduma za afya nchini kuhusu Saratani.
Aidha, kuanzishwa kwa huduma za upimaji wa saratani katika Hospitali na vituo vya afya zaidi ya 300 nchini na huduma za Tiba kupitia Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.
“Serikali itapanua wigo wa matibabu ya saratani katika Hospitali ya Bugando Mwanza na KCMC, Kilimanjaro. Mipango ya baadae ni huduma hizo pia kutolewa ktk Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.”hii itapunguza wagonjwa kufuata huduma kwenye hospitali ya saratani ya Ocean Road
Mkutano wa 10 wa Saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unafanyika kwa kuasisiwa kwa juhudi za wake za Marais wa bara la Afrika.
Mkutano huu unahudhuriwa na Wake wa Marais wa Afrika, Mawaziri wa Afya wa Afrika, Wanataaluma na Wadau wa Maendeleo. Lengo kuu ni kufanya mapitio ya hatua zilizochukuliwa na nchi za Afrika, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya pamoja na ya nchi katika kukabiliana na saratani.
Wakati wa kukabidhiwa uenyekiti wa Umoja wa Wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na saratani ya Shingo ya Kizazi, Matiti na Tezi Dume kutoka kwa Mwenyekiti anaemaliza muda wake, mke wa Rais wa Kenya mama Magreth Kenyatta, Mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia mama Roman Tesfaye Abneh ameleeza masikitiko yake kwa jinsi ambavyo ugonjwa wa saratani unavyoua kuliko hata ugonjwa wa UKIMWI na kifua kikuu. Hivyo ameziomba nchi za Afrika kuongeza uwekezaji katika eneo hili hasa kwa kuhakikisha dawa zinakuwepo za kutosha, kuboresha utoaji wa huduma za afya ikiwemo upimàji na tiba, kuhakikisha nchi zinatoa mafunzo ya Kutosha kwa watumishi  wa afya katika fani hii

0 maoni:

Chapisha Maoni