Mgombea urais wa chama cha
Republican nchini Marekani Donald Trump ameahidi kumaliza uhalifu na
ghasia nchini Marekani iwapo atachaguliwa kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu
mwezi Novemba.
Akiongea katika kongamano kuu la chama cha
Reublican wakati wa hotuba yake ya kukubali uteuzi, mgombea huyo amesema
hakuwezi kuwa na ufanisi bila kuwepo utawala wa sheria.
Aidha,
ameahidi kuchukua hatua kali kukabiliana na wahamiaji haramu na akaonga
kuwa kwa sasa wahamiaji wanaruhusiwa kuingia na kuishi katika jamii za
Marekani bila kuzingatia usalama wa umma.
- Wanawe Trump wafana kongamano la Republican
- Mambo 20 makuu anayoamini Donald Trump
Bw Trump amejieleza kama mkombozi na sauti ya wanyonge na watu
waliosahaulika nchini Marekani, na akajionyesha kama mtu mwenye sifa
tofauti na mpinzani wake wa chama cha Democratic Hillary Clinton ambaye
sana amemuonesha kama mtu mfisadi na asiyewajibika.
Mfanyabiashara
huyo tajiri kutoka Marekani amesema atakomesha sera ya kujenga mataifa
na kufanikisha mageuzi ya serikali katika nchi nyingine ambayo amesema
imefeli.
Amesema sera hiyo ndiyo chanzo cha matatizo yanayoshuhudiwa nchini Iraq, Libya, Misri na Syria.
- Trump anafanana na Hitler, Rais wa Mexico asema
Ameahidi kufanya kazi na washirika wote wa Marekani wanaotaka kuangamiza kundi la Islamic State.
0 maoni:
Chapisha Maoni