Jumatatu, 25 Julai 2016

HUKUMU YA ASKARI POLISI ALIYEMUUA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI INATOLEWA KESHO JULAI 27

Postedy by Esta Malibiche on July 26 in JAMII with No comments












Ulinzi  wa  polisi  viwanja  vya mahakama  kuu kanda  ya  Iringa  leo  kabla ya  mtuhumiwa wa mauwaji  kufikishwa
Wananchi  wakiwa  foleni  kukaguliwa  kabla ya  kuingia  mahakamani leo
Mtuhumiwa wa  mauwaji  ya  Mwangosi  akipakiwa  kwenye  gari  za  FFU
Msafala  wa  gari  za  FFU  zilizomsindikiz askari  mwenzao anayekutwa  na kosa  la  kuua bila  kukusudia  leo
Askari  wa FFU  wakitoka  mbio  mahakamani  hapo
Wananchi  na  wanahabari  wakitoka  mahakamani  hapo 


MAHAKAMA  kuu kanda ya Iringa  imemtia hatiani Askari Polisi wakikosi cha Kuzuia Ghasia cha Mkoani hapa (FFU) Pisificus Saimoni anayetuhumiwa kumuua   aliyekuwa Mwandishi  wa habari wa kituo cha Channel Ten mkoani hapa Daud Mwangosi kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Akisoma mwenendo  wa kesi hiyo jana Jaji wa mahakama kuu kanda ya Iringa  Dk Paul Kihwelo  alisema mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa kufuatia ushihidi wa ungamo alioutoa mwenyewe mbele ya mlinzi wa amani.

Alisema katika ushahidi huo uliotolewa mahakamani hapo na mlinzi wa amani ambaye pia upande wa Jamuhuri ulitoa kielelezo cha ungamo hilo kama kidhibiti namba 3 katika kesi hiyo na kupokelewa na mahakama,mtuhumiwa alikiri kutendo kosa hilo bila kukusudia.

Jana ilikuwa siku yakusonmwa   kesi hiyo iliyudumu kwa kipindi cha miaka minne lakini           jaji Dk   Kihwelo alilazimika kuahirisha kutokana na mvutano uliotolewa na mawakili wa pande zote mbili jamuhuri na utetezi.

Katika maelezo yake Mwanasheria mwandamizi wa serikali Aldof Maganda alisema.”Ahasante Mheshimiwa …kwakuwa mahakama yako tukufu imemtia hatiani kwakosa dogo la kuua bilakukusudia”alisema na kuongeza:

“Basi tunaomba mahakama yako imuhukumu mtuhumiwa kifungo cha masisha jela kwa kutumia kifungu cha  198 cha sheria ya Makosa ya jinai na kanuni ya adhabu sura ya 16  kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002”alisema Maganda.

Naye Wakili wa utetezi katika kesi hiyo Rwezaula Kaijage alitoa sababu tano za kuishawishi mahakama kumuonea huruma mtuhumuwa huyo na kumpunguzia adhabu kwa kumuachia huru kwa masharati maalum.

“Mtuhumiwa nikijana wamiaka 27 bado ni nguvu kazi ya taifa,pia Septemba 2 mwaka 2012 siku ambayo tukio lilitoikea mtuhumiwa alikwenda si kwa ridhaa yake bali alikuwa akitekeleza amri na sheria”alisema Kaijage na kuongeza:

“Mtuhumiwa pia amekaa mahabusu kwa kipindi cha miaka minne,wazazi wake wote wawili wamefariki na yeye ndiyo tegemeo kwa familia yao yenye watoto watano na pia anamtoto mmoja,kwa shufaa zote hizo tunaomba mahakama yako impunguzie adhabu kwa kumuachia huru kwa masharti”alisema Kaijage.

Akiahirisha kesi hiyo jaji Kihwelo alisema;”Nimesikiliza pande zote mbili ,upande wa jamuhuri ukitaka mtuhumiwa apewe adhabu ya kifungo cha maisha jela,na upande wa utetezi ukitaka aachiwe huru kwa masharti…ninaahirisha shauri hili hadi Julai 27,nitakapokuja kusoma hukumu”alisema.

Awali akisoma mwenendo wa kesi hiyo jaji Kihwelo alisema katika shauri hilo upande wa Jamuhuri ilishindwa kuwafikisha mahakamani mashahidi muhimu akiwamo ili kuthibitisha za kua bilakukusudiwa iliyofikishwa mahakamani akiwamo Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa wawakati huo Michael Kamuhanda na RCO wawakati ule  Nyegesa Wankyo.

“Sheria inataka upande wa jamuhuri kuthibitisha pasipo shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa bila yashaka yoyote,na katika ushahidi ulioletwa mahakamani upande wa Jamuhuri haukuleta mashahidi muhimu”alisema.

Jaji Kihwelo alisema katika kesi hiyo upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne na vielelezo vitano vilivyopokelewa na mahakama huku akieleza kuwa kielezo namba moja ambacho ni gazeti la Mwananchi kilipokelewa kama utambulisho lakini hakikupokelewa kamakithibiti kutokana na kuto kidhi vigezo vya kisheria.

Jaji Kihwelo alisema kielelezo hicho kilishindwa kidhibiti  kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo upande wa Jamuhuri kushindwa kumfikisha mahakamani mtu aliyepiga picha hiyo kutoa ushahidi mahakamani.

0 maoni:

Chapisha Maoni