Postedy by Esta Malibiche on july 18 News
Balozi
Ombeni Sefue akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Taifa wa Utafiti wa
Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wakati
alipofanya ziara katika taasisi hiyo mwishoni mwa wiki ili kujionea
shughuli mbali mbali zinazofanywa na taasisi hiyo.
Kwa
kiwango kikubwa (NHBRA) imeonyesha ni taasisi inayoweza kujenga nyumba
za bei nafuu sana hasa vijijini ili watanzania wa maeneo hayo waweze
kupata makazi bora ya kuishi kwa bei rahisi zaidi, Kulia katika picha
ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Matiko Samson Mturi.
Taasisi
hiyo pia imekuwa ikijihusisha na mafunzo teknolojia ya ujenzi wa nyumba
za bei nafuu kwa vikundi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na
kuwafundisha juu ya utengenezaji wa matofali, vigae vya kuezekea nyumba
pamoja na ujenzi wa nyumba za zenyewe ambapo taasisi na wananchi
mbalimbali wanaweza kufaidika na mpango huo nchini.
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na shughuli za kutengeneza vigae vya kuezekea nyumba katika karakana ya taasisi hiyo.
Balozi
Ombeni Sefue akitembezwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Matiku Samson
Mturi maeneo mbalimbali ili kujionea shughuli za zinazofanywa na
taasisi hiyo.
Balozi Ombeni Sefue akiangalia wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati wakitengeneza vigae kwa ajili ya kuezekea nyumba.
Balozi
Ombeni Sefue akipiga picha kwa simu yake huku wafanyakazi wa taasisi
hiyo wakimuangalia baada ya moja ya nyumba ndogo iliyojengwa katika
ghala ya taasisi hiyo kwa ajili ya mfano kumfurahisha.







0 maoni:
Chapisha Maoni