Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wapili kulia)
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu (BAKWATA),
Suleman Said Lolila wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika Hoteli
ya Serena, Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Viongozi
wa Dini lililojadili masuala ya ugaidi. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba, na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na viongozi
wa dini kuhusu masuala mbalimbali ya amani nchini katika Kongamano la
Viongozi wa Dini lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es
salaam. Katika hotuba yake, Waziri Mwigulu aliwataka viongozi hao
kutokuhusisha kosa lifanyalo na mtu au watu fulani kulifananisha na dini
yake, amewaomba viongozi hao watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa za
matukio mbalimbali ya kiuhalifu nchini. Kutoka kulia ni Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Paul Ruzoka, Mufti Mkuu wa Tanzania,
Abubakary Zubeiry Bin Ally na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo
Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita.
Sehemu
ya viongozi wa dini walihudhuria katika Kongamano la Viongozi wa Dini
nchini lililofanyika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kongamano
hilo ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu
M.L Nchemba (hayupo pichani), lilijadili masuala mbalimbali ya ugaidi
pamoja na ushirikiano wa dini mbalimbali nchini. Hata hivyo Waziri
Mwigulu aliwataka viongozi hao kutokuhusisha kosa lifanyalo na mtu au
watu fulani kulifananisha na dini yake, amewaomba viongozi hao watoe
ushirikiano kwa kutoa taarifa za matukio mbalimbali ya kiuhalifu nchini.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (watatu kulia) akiandika
maelezo ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT),
Dk Leonard Mtaita (kushoto) katika kongamano la viongozi wa dini
lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kongamano
hilo lilijadili kuhusu ugaidi na ushirikiano wa madhehebu mbalimbali ya
dini nchini. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Mstaafu, Alex
Malasusa. Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry Bin Ally (wapili
kushoto), Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Paul Ruzoka (watatu
kushoto) na Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba
akimfafanulia jambo Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry Bin Ally
(kushoto) mara baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L
Nchemba (hayupo pichani) kuzungumza na viongozi wa dini kuhusu masuala
mbalimbali ya amani nchini katika Kongamano la Viongozi wa Dini
lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Afisa Sheria wa Wizara hiyo, Berious Nyasebwa.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni