Wazee hao waliyasema hayo hivikaribuni wakati Jaji wa mahakama hiyo, Paul Kiwelo akihitimisha usikilizwaji wa shauri hilo ambalo hukumu yake ataitoa KESHOKUTWA Julai 21, mwaka huu.
“Niwashukuru mawakili wa utetezi na Jamuhuri, niwashukuru watu wote waliokuwa wakiudhuria kesi hii tangu ianze mpaka leo inapohitimishwa kwa ajili ya hukumu itakayotolewa Julai 21, mwaka huu,” Jaji Kiwelo alisema.
Kwa mara ya kwanza Simoni alifikishwa mahakamani hapo Septemba 12, 2012 akituhumiwa kumuua Mwangosi kwa kukusudia katika tukio lilitokea katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi Mkoani Iringa Septemba 2, 2012 wakati mwandishi huyo alipokuwa akiwajibika katika kazi zake za kutafuta habari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
0 maoni:
Chapisha Maoni