Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla amekutana na Wakuu wa Idara za Maenedeleo ya Jamii pamoja
na ile ya Watoto katika Wizara hiyo na kupanga mikakati mbalimbali ya
kiutendaji kazi.
Katika
tukio hilo, Dk. Kigwangalla amewataka wakuu hao wa Idara kuhakikisha
wanaandaa mpango kazi kabambe ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi
ndani ya Wizara hiyo ikiwemo kutoa maagizo maafisa Maendeleo ya na
Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanatoka maofisini na kwenda ngazi ya chini
kufanya kazi hasa Vijijini.
Pia
katika kukabiliana na suala la mmong’onyoko wa maadili hasa suala la
vitendo vya watu kujihusisha na mapenzi ya Jinsia moja, amebainisha kuwa
mikakati hiyo kwa sasa wataanzia ngazi ya chini katikakuhakikisha
wanadhibiti vitendo hivyo.
“Tunataka
kuhakikisha vitendo vya unyanyasi na ukatili hasa vile vinavyoanzia
mashuleni tunavikomesha mara moja. Imebainika zipo baadhi ya shule
watoto wanafanya vitendo visivyo fa ambavyo pia baadae vinapelekea tabia
hii ya ushoga.
Hivyo
miongoni mwa mikakati ni kuhakikisha tunaandaa masunduku ya maoni kwa
kila shule ili kubaini vitendo hivi na vingine visivyofaa kwa Wanafunzi
ambavyo vinapelekea mmong’onyoko wa maadili.” Alieleza Dk. Kigwangalla.
Dk.
Kigwangalla amekutana na wakuu hao ni katika mikakati ya kuhakikisha
anasimamia ipasavyo majukumu ya Idara hizo ambazo zinaunda Wizara hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akipitia madokezo mbalimbali ya Idara za Wizara hiyo muda
mfupi kabla ya kukutana na Wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na ile
Idara ya Watoto.
Afisa
wa Idara ya Watoto, Emmanuel Batoni akielezea jambo kwa Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla (Hayupo pichani) wakati wa tukio hilo lililofanyika katika
ukumbi wa Wizara hiyo.
Mkutaano
huo wa Naibu Waziri na Wakuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na ile ya
Watoto ukiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla
Sehemu
ya Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akitoaa maagizo kwa Wakuu wa Idara mbalimbali wa Wizara
hiyo.(Picha zote na Andrew Chale,).
0 maoni:
Chapisha Maoni