Jumatano, 20 Julai 2016

WAZEE WA WILAYA YA IKUNGI WAMKUBALI DC MTATULU , AWAAHIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII

Posted by Esta Malibiche  on July 20 in News

Dc Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kikao

Mtaturu akisikiliza kwa makini moja ya ushauri uliopatiwa na wazee baada ya kikao kumalizika 
  
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na wakuu wa idara Wilayani humo wakisikiliza kwa lakini maelekezo ya kiutendaji
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji J. Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na wazee waliowawakilisha wazee wengine wilayani humo
 
Na Mathias Canal, Singid
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu amekutana na zaidi ya wazee 137 kutoka vijiji 101 vilivyopo katika Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida.
Katika mazungumzo ya mkuu huyo wa Wilaya na wazee hao yalijikita zaidi katika kujadili namna ya kukabiliana na umasikini kupitia nguvu Kazi ya Taifa (Vijana) katika kilimo na ufugaji wa kisasa.
Dc Mtaturu amewasilisha dhamira ya serikali ya Hapa Kazi Tu chini ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Joseph Pombe Magufulu kwa wazee wa Wilaya ya Ikungi na Taifa kwa ujumla ni kupambana na mafisadi, Rushwa na wahujumu uchumi ili kuboresha huduma za Jamii ikiwemo Afya hususani katika kuboresha huduma za Afya kwa wazee wote nchini sawia na Wanawake wajawazito na watoto.
Katika kuhakikisha kunakuwa na chachu ya maendeleo kwaMapinduzikubwa Wilayani humo Mtaturu alisema kuwa serikali imekusudia kuboresha kilimo na ufugaji ili viwe vya tija na kibiashara na kupelekea kupunguza umasikini wa wananchi mwaka hadi mwaka.
Mtaturu anakuwa Mkuu wa Wilaya wa kwanza kukutana na kundi la wazee Siku chache baada ya kuapishwa jambo ambalo halijawahi kutokea kwa kiongozi mwingine yeyote Wilayani humo tangu Mkoa wa Singida ulipoanzishwa.
Kwa upande wao wazee hao wameonyesha wazi mapenzi yao ya dhati kwa mkuu huyo wa Wilaya na kuahidi ushirikiano uliotukuka katika utendaji wake.
Wakati huo huo wazee hao wamemshukuru Mh Rais Magufuli kwa uteuzi alioufanya kumpeleka Mkuu huyo wa Wilaya kuongoza wananchi hao ambao wameonyesha kukatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wa serikali wilayani humo ambao wameshindwa kutatua changamoto za wananchi.
Awali Dc Mtaturu alikuwa na kikao cha mapema na watumishi wa Halmashauri na wakuu wa idara ili kukumbushana majukumu ya kila mmoja utendaji wake na kuwasihi kufanya Kazi kwa bidii zaidi kwa kushirikiana na wananchi.
Mtaturu amewakumbusha watumishi hao wajibu wao wa kusimamia miradi ya maendeleo kwa kupata thamani halisi ya fedha (Value for Money) kushughulika na kero za wananchi ikiwemo kutafsiri ilani ya Uchaguzi kwa vitendo ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewapa muda wa mwezi mmoja watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wanaoishi Singida Mjini takribani kilomita 41 kutoka Wilayani hapo wawe wamehamia Wilayani Ikungi kwani amebaini ni watumishi wanne pekee ndio wanaoishi Wilayani hapa jambo ambalo linapunguza ufanisi wa Kazi.

Katika sekta ya michezo Mtaturu alisema kuwa ili kuibua vipaji na Mkoa wa Singida kwa muda mrefu umekuwa na Sifa ya kutoa wanariadha hivyo ili kuenzi heshima hiyo anataraji kuanzisha Ikungi Marathon ili kuwapa fursa Vijana wenye vipaji kuibuka na kufika mbali zaidi katika medani za Riadha

0 maoni:

Chapisha Maoni