SERIKALI,imesema kuwa kinu cha kusaga mazao cha shirika la
taifa la usagishaji,NMC ,cha Arusha hakijauzwa kama ilivyoenezwa na
kitaendelea kuwa mali ya serikali na kwamba anaendesha kinu hicho ni
mpangishaji na si vingine.
Hayo yameelezwa na msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru,
alipokuwa akikabidhi umiliki wa kinu hicho cha kusaga nafaka cha NMC
,cha Arusha kutoka kwa shirika hodhi la mali za serikali, CHC,kwenda kwa
bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko. .
Mafuru, amesema uamuzi huo wa kukabidhi umiliki wa kinu
hicho kwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ni maelekezo ya serikali
kwa ajili ya kukiendeleza kinu hicho na vingine vilivyopo, Mwanza,
Iringa na Dodoma.
Amesema kuwa bodi hiyo ambayo ni mmiliki mpya itakuwa na
jukumu la kukiendesha kinu hicho itapitia mkataba wa upangaji na
kampuni ya uwekezaji ya Monaban Trading Company limited kwa kuwa hiyo ni
sehemu ya biashara.
Amesema kabla ya kukikabidhi kinu hicho kwa mmiliki mpya walijiridhishwa kwa kufanya uhakiki wa vitu vilivyopo.
Mafuru,amevitaja vinu vingine ambavyo havitabinafisishwa na
vitabakia kuwa ni mali ya serikali ni pamoja na shirika la usagishaji
la taifa NMC, Mwanza, NMC,Dodoma na NMC,Iringa ,ambavyo navyo
vimekabidhiwa kwa mimiliki mpya ambayo ni bodi ya nafaka na mazao
mchanganyiko.
Ameongeza kuwa kinu hicho cha NMC ,Arusha, kilipangishwa
mwaka 2008 kwa kampuni ya Monaban Trading limited,kutokana na uamuzi wa
serikali uliofanywa kwa wakati huo lakini sasa mali zote za shirika la
usagishaji la taifa hazitauzwa zitabakia kuwa mali ya serikali.
Nae Kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya nafaka na mazao
mchanganyiko, John Damasi Maige, amesema bodi hiyo itasimamia shughuli
zote za kinu hicho pia watazingatia mkataba unaomwezesha mpangaji
kampuni ya Monaban kuendesha kinu hicho.
Amesema kuwa mara baada ya kupitia mkataba na mpangaji
ambae ni kampuni ya Monaban Trading Compan Limited,kuna mambo
watakubaliana kwa masilahi ya pande zote mbili.
Maige, amesema kuwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko
inaendesha maghala yaliyopo Dodoma, na kufufua mashine za kusagisha
zilizopo NHC Mwanza,ambacho kilikuwa ni kwa ajili ya kusagisha na
kusindika mpunga, kinu cha Dodoma kilikuwa cha kusagisha na kusindika
mtama .
Lengo la kuvifufua ni kuviwezesha kufanya kazi na hivyo kutoa ajira hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Monabani
Trading Limited, Gerad Mandala, amesema watashirikiana na mmiliki mpya
kwa kuwa kinu hicho ni mali ya serikali na kiwanda kitaendelea kama
kawaida.
Akawaondoa hofu wananchi kwa kueleza kuwa kampuni ya
Monaban ni mpangaji na ina mkataba wa muda mrefu na itaendelea kuwa
msagishaji wa nafaka na mazao mengine hivyo wananchi wataendelea kupata
huduma ya unga na mahitaji mengine kama kawaida..
0 maoni:
Chapisha Maoni