Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiwa katika
picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,
Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande
hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa
serikali kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kulia), akiwa
katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (kushoto), Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kushoto) na Mwakilishi Mkazi
wa AfDB, Tania Kandiero (wa tatu kushoto), baada ya kumalizika kwa
mazungumzo kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi
kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha
shilingi 433.6bn.Picha Zote na Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), akipeana mkono na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika -AfDB, Tania Kandiero,
alipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, kwa
mazungumzo maalumu, akiwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic
Kacou, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa
serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto),
akimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic
Kacou (katikati) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini
Tanzania, Tania Kandiero (kulia) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia
Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi
433.6bn. Aliyeketi kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Kushoto)
akibadilishana “Business Card” na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo
kati ya pande hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko
Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akifuatilia kwa
makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,
Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani) ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia
Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi
433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), (Katikati), akiwa
katika mazungumzo maalumu na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou, katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi yake
Jijini Dar es slaam, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa
Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn
Kaimu
Kamisha Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta
Mtagwaba akifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb), na Makamu wa Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika-AfDB, Dkt. Alberic Kacou (hawapo pichani), ambapo
Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka
2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akibadilishana
“Business Card” na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,
Dkt. Alberic Kacou, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya pande
hizo mbili, ambapo Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa
serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa katika mazungumzo
maalumu na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, ukiongozwa
na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt. Alberic Kacou, aliyeambatana na
Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini Tanzania, Tania Kandiero, ambapo
Benki hiyo imeahidi kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka
2016/2017, kiasi cha shilingi 433.6bn.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (Kushoto)
akizungumza jambo wakati alipokutana na ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo
ya Afrika-AfDB, ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo, Dkt.
Alberic Kacou (katikati) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo
nchini Tanzania, Tania Kandiero (kulia) ambapo Benki hiyo imeahidi
kuchangia Mfuko Mkuu wa Bajeti wa serikali mwaka 2016/2017, kiasi cha
shilingi 433.6bn.
Na Benny Mwaipaja-WFM
BENKI
ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, imeahidi kuchangia Dola Milioni 200, sawa
na Shilingi 433.6b, kwenye Mfuko wa Bajeti Kuu ya Serikali katika
kipindi cha mwaka wa Fedha 2016/2017.
Ahadi
hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anayeshughulikia Utawala
na Rasilimali watu, Dkt. Alberic Kacou, alipomtembelea Waziri wa Fedha
na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Ofisini Kwake Jijini Dar es salaam
Makamu
huyo wa Rais wa AfDB aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo,
Tania Kandiero, amesema kuwa mchango huo umeongezeka kwa dola Milioni 50
ikilinganishwa na Bajeti ya mwaka jana ambapo Benki hiyo ilichangia
Dola Milioni 150. “Misaada na mikopo inayotolewa na Benki yetu kwa
serikali ya Tanzania imefikia Dola za Marekani 1.9b hivi sasa” Alieleza
Dkt. Kacou
Ameeleza
kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza katika Bara la Afrika kupewa kiasi
kikubwa cha fedha kutokana na mipango yake mahili ya maendeleo
inayokidhi vigezo na viwango vya taasisi hiyo. “Tuna malengo matano
ambapo tunataka kuwekeza katika sekta ya nishati, uzalishaji wa chakula,
kuiendeleza kiviwanda, kuiunganisha na kuboresha maisha ya waafrika kwa
ujumla” aliongeza Dkt. Kacou
Amepongeza
jitihada zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na
Rais Dkt. John Magufuli, kwa kusimamia vizuri nidhamu ya matumizi ya
fedha za umma na kwamba uamuzi huo utaharakisha maendeleo ya nchi.
Akizungumza na ujumbe huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, ameshukuru uamuzi wa Benki hiyo wa kuongeza mchango wake katika
Bajeti Kuu ya serikali kupitia mfuko mkuu wa Bajeti (GBS).
Amesema
kuwa serikali imedhamiria kutekeleza mipango yake ya ujenzi wa reli ya
kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge), pamoja na kununua ngege
tatu za abiria ili kuboresha usafiri wa anga.
“Vilevile
tumeamua katika Bajeti ya mwaka huu kununua meli mpya itakayo tumika
kutoa huduma Ziwa Viktoria na kukarabati meli nyingine mbili ambapo moja
iko Ziwa Tanganyika na nyingine Ziwa Viktoria ili kuimarisha usafiri wa
majini” Aliongeza Dkt. Mpango
Dkt.
Mpango amebainisha kuwa katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa
Maendeleo, serikali imejipanga kukuza sekta ya viwanda ili kuiwezesha
nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. “Mpango huo utakwenda
sambamba na kuboresha sekta ya kilimo ili malighafi itakayozalishwa na
wakulima, licha ya kuinua uchumi wa wakulima wetu, lakini pia viwanda
vitapata malighafi ya kutosha” alisisitiza Dkt. Mpango
Amerejea
msimamo wa serikali kuwa haitakubali kupokea misaada inayoambatana na
masharti magumu na isiyo na tija kwa nchi na kwamba jitihada
zinazofanyika hivi sasa ni kuhakikisha kuwa rasilimali zilizopo nchini
zinawekezwa kwa utaratibu mzuri ili ziweze kutumika kuleta maendeleo.
“Hatutakubali
misaada isiyozingatia vipaumbele vyetu na ile inayohatarisha uhuru wetu
wa kujiamulia mambo yetu wenyewe” alieleza Dkt. Mpango.Ameeleza kuwa
uamuzi wa serikali wa kukusanya mapato yake ya ndani kwa kuwahimiza watu
kulipa kodi na kubana matumizi yasiyo ya lazima umeanza kuleta matunda
na kuongeza pia nidhamu ya matumizi ya pesa katika jamii.
Ameiahidi Benki hiyo ya maendeleo ya Afrika-AfDB, kwamba fedha waliazoahidi kuzitoa zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni