Jumatatu, 25 Julai 2016

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MAADHIMISHO KUMBUKUMBU YA MASHUJAA MJINI DODOMA

shuj2Msafara wa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Mashujaa tayari kwa maadhimisho hayo yaliyofanyika  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa  mjini Dodoma leo Julai 25, 2016 (PICHA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA NA IKULU)
shuj4Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Mashujaa tayari kwa kuongoza maadhimisho hayo yaliyofanyika  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa  mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj2Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiielekea kwenye mnara wa kumbukumbu tayari kwa kuongoza maadhimisho ya mashujaa  katika Mnara wa kumbukumbu wa Mashujaa  mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj8Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akitoa heshima mara baada ya kuweka Sime na ngao  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj6Baadhi ya askari wa vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama vikiwa vimejiweka tayari kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu  ya mashujaa iliyoadhimishwa leo kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma.
shuj7Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akielekea kwenye mnara tayari kwa  kuweka Sime na ngao  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj1Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akikabidhiwa  Sime ili kuweka  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj9 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka Sime katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj8Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akitoa heshima mara baada ya kuweka Sime na ngao  katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj9shuj4Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa wamesimama na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma leo.
shuj1Viongozi mbalimbali wa serikali,vyama vya siasa wakiwemo wabunge wakiwa  katika maadhmisho hayo mjini Dodoma leo.
shuj5Kutoka kulia ni Mke wa Rais Mama Janet Magufuli, Mwenyekiti wa TLP Bw. Agustino Mrema. Spika mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Amer Pandu Kificho, Waziri wa mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba. Waziri wa Ulinzi Dk. Hussein Mwinyi, Mwanasheria mkuu wa Serikali Mh. George Masaju na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakiwa katika maadhimisho hayo.
shuj7Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
shuj11Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika  Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
1Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika  Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016
maj1Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi katika maadhimisho hayo.
shuj13Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 20
shuj10Baadhi ya wananchi wakishangilia wakati Rais Dk. John Pombe Majaliwa alipokuwa akizungumza katika maadhimisho hayo.
shuj12 Baadhi ya viongozi waliohudhuria maadhimisho hayo wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wakati alipokuwa akiwasalimia wakazi wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo kutoka kushoto ni Naibu Spika Tulia Akson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar   Mhe Mohammed Said Mohammed Dimwa, Mke wa Rais Mama Janet Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwa katika maadhimisho hayo.
……………………………………………………………………………………………
Na: Immaculate Makilika- Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa watanzania kudumisha amani iliyopo ambayo ilipatikana baada ya Mashujaa mbalimbali kuipigania na hata kujitoa uhai wao kwa ajili ya Taifa.
Akizungumza leo, wakati akihutubia wananchi mara baada ya kumaliza shughuli za maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Mashujaa  iliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo mjini Dodoma.
Rais Magufuli alisema kuwa maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa  ni muhimu kwa vile watu hao walijotoa kwa ajili ya kulitetea taifa.
“Wakati tunawakumbuka waliotangulia mbele za haki, sisi tuliobaki tudumishe amani hii, kama ambavyo wao waliotutangulia hawakujali dini zao bali taifa hili” alisema Rais Magufuli.
Aliongeza kuwa nchi ya Tanzania imebaki kuwa kisiwa cha amani, na amani hiyo isichezwe  bali ijengwe na kudumishwa kwa umoja na mshikimamano ili kusaidia kuitangaza nchi zaidi.
Aidha, viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Ali Mohamedi Shein, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili  Mheshimiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa John Samweli Malecela nao wapewa fursa ya kuzungumza na wananchi kuhusu maadhimisho hayo ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
Viongozi hao, wamesisitiza umuhimu wa kudumisha amani iliyopo na kusema kuwa ni jukumu la wananchi  wote kuhakikisha  hawashiriki katika vitendo vitakavyosababisha   uvunjifu wa amani.
Ambapo, waliwataka wananchi kuwaombea Mashujaa wote waliofariki katika vita mbalimbali wakiwa  katika  harakati za kulifanya Taifa la Tanzania kuwa huru.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, alisema kuwa atahakikisha anasimamia utekelezaji wa agizo la Rais la kuitaka Serikali kuhamia mjini Dodoma.
“Nahamia Dodoma mwezi wa tisa,na nitakapohamia mawaziri wote lazima wanifuate. Katika hili nitasimamia kwa nguvu zote” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Awali, Mheshimiwa Rais Magufuli alisema kuwa atahakikisha katika kipindi cha utawala wake, Serikali inahamia mjini Dodoma, kwa vile Rais wa Awamu ya kwanza Mwl. Julius Nyerere alionesha nia ya kufanya hivyo.
 Aliongeza  kuwa  kwa sasa mji wa Dodoma unaweza kukidhi mahitaji hayo ya Serikali kwa kutumia  miundombinu iliyopo, hata hivyo Serikali inaendelea kujenga miundombinu mipya.
Maadhimisho ya kumbukumbu za Mashujaa hufanyika Julai 25, ya kila mwaka, kwa   kufanya  maombolezo ya Mashujaa waliopigana katika vita mbalimbali katika harakati za kutetea uhuru wa nchi ya Tanzania.
Maadhimisho ya mwaka huu yamefanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma, ambapo Rais John Pombe Magufuli alikuwa mgeni rasmi, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuhudhuria maadhimisho hayo kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

0 maoni:

Chapisha Maoni