Postedy by Esta Malibiche on July 20News
Naibu waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo |
NaibuWaziri Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Kilolo |
Watumishi wa Halmashauri ya Kilolo wakimsikiliza kwa makini Naibu waziri |
Naibu waziri akikagua vyumba vya bweni la wavulana shule ya sekondari Kilolo |
Waziri akiwa katika zahanati ya kituo cha Afya kilolo |
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo amebariki mchakato wa Wilaya ya Kilolo wa kutaka kuigawa Halmashauri hiyo kuwa Halmashauri mbili.
Kwa sasa halmashauri
hiyo imezaa mji mdogo wa Ilula ambao kwa sasa unapiganiwa na serikali ya mkoa
pamoja na wadau mbalimbali kufikia hadhi ya kwua Halmashauri.
Akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kaatika kijiji cha Nyanzwa katika mji wa Ilula
Jafo alikokwenda kutembelea mradi wa kilimo cha umwagiliaji alisema kutokana na
jiogorafia ya Wilaya hiyo wazo la kuugawa mji huo ni wazao sahihi.
Mchakato wa kutaka
Halmashauri ya Kilolo kugawanywa uliibuka miaka mitatu iliyopita na tayari
vikao mbalimbali vikiwamo ile vua ushauri vya Wilaya (DCC)na Mkoa
(RCC)vimepitisha pendekezo hilo na kuliwasilisha ofisi ya Tamisemi yenye jukumu
la kufikia uamuzi.
“Ofisi yangu imepokea
maombi ya kutaka kugawanywa kwa Halmashauri ya kilolo,na tayari mda si mrefu
wataalamu wangu watakuja kwa lengo la kukagua na kuona kama unakidhi sifa za
kugawanywa”alisema Jafo na kuongeza:
“Lakini niseme hata
wataalamu wakija na kutoa mapendekezo tofauti kuwa mji haujafikia hadhi hiyo
ama ya bado mdogo mimi mwenyewe nitasema mbona nimefika huku na kujionea
halihalisi”alisema.
Alisema kwa halihalisi
ya jiografia ya Wilaya hiyo ni dhahiri inawawi vigumu watu wa upande wa Ilula
kwenda kufuata huduma za kiutawala umbali wa zaidi ya KM 100 yalipo makao makuu
ya Wilaya na Halmashauri ya wilaya hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah alisema ofisi yake imejipanga kuhakikisha
inatekeelza maelekezo yote yanayotolewa na serikali kuu ili kuhakikisha
wananchi wanapata maendeleo.
“Mheshimiwa Naibu Waziri
sisi tumejipanga vizuri na tunakuhakikishia tupo pamoja na tupo tayari
kutekeleza maelezo yote kutoka serikali kuu kwa ajili ya kuwaletea wakazi wa
Kilolo maendeleo.
Mbunge wa Jimbo hilo
Venance Mwamoto alisema kutimizwa kwa ahadi ya kuigawa Halmashauri ya Kilolo
kutasaidia wananchi kufikiwa na Huduma muhimu za kijamii.
0 maoni:
Chapisha Maoni