Jumatatu, 25 Julai 2016

MABONDIA WA KIKE KUPANDA ULINGONI AGOST 7 UWANJA WA TAIFA KUWASINDIKIZA GALILE NA KALAMA


Promota wa mchezo w masumbwi nchini  Haruna Mussa ‘Dippo’  katikati akizungumza na mashabiki wa mchezo wa ngumi za kulipwa wakati alipowatambulisha kupigana kwa mabondia wa kike Halima Bandola na Joyce Awino watakao oneshana umwamwamba Agost 7 katika uwanja wa ndani wa  Taifa.
Promota wa mchezo w masumbwi nchini  Haruna Mussa katikati akiwainua juu mabondia mbele ya mashabiki wa mchezo wa ngumi za kulipwa wakati alipowatambulisha kupigana kwa mabondia wa kike Halima Bandola na Joyce Awino watakao oneshana umwamwamba Agost 7 katika uwanja wa ndani wa  Taifa .
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA wa kike katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Halima Bandola na Joyce Awino watapanda uringoni Agost 7 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa akizungumza na mashabikiwa mchezo wa masumbwi wishoni mwa wiki iliyopita promota wa mpambano uho Haruna Mussa ‘Dippo’
amesema ameamua kuwa promoto watoto wa kike kwa ajili ya kuhamasisa wasichana kuupenda na kuucheza mchezo wa masumbwi kwani kwa sasa michezo ni ajira kwa vijana aliongeza kwa kusema katika mpambano uho kutakuwa na mpambano wa kukata na shoka mabondia Kalama Nyilawila atavaana na Selemani Galile mpambano wa raundi kumi katika uzito wa kg 72
wakati mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Meshack Mwankemwa kutoka Mbeya atakumbana na Selemani Zugo mpambano wa ubingwa wa KG 66 raundi kumi Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  ‘Super D’ kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi

0 maoni:

Chapisha Maoni