Afisa
Mwandamizi kutoka Kitengo cha Elimu katika Jeshi la Polisi kikosi cha
usalama barabarani , ASP. Mossi Ndozero akitoa Elimu ya usalama
barabarani kwa baadhi ya walimu wa shule za Mkoa wa Mwanza yaliyofanyika
katika Chuo cha Polisi Wanamaji jijini Mwanza yaliyoendeshwa na jeshi
hilo chini ya udhamini wa kampuni ya TBL Group.
…………………………………………………………………………………………………….
Kampuni ya TBL Group imetangaza
kuwa itaendelea kutoa elimu ya Usalama katika maeneo yake ya kazi na
kwa jamii ili kuhakikisha matukio ya ajali zisizo za lazima zinapungua
hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa
Usalama kazini wa kiwanda cha TBL cha mjini Mwanza,Bw.Method Marco
wakati akielezea mafunzo ya usalama ambayo yamefadhiliwa na kampuni kwa
ajili ya walimu wa shule za msingi na sekondari na wakaguzi wa magari
kutoka Jeshi la polisi nchini mkoani humo.
Bw.Method alisema linapokuja
suala la usalama na afya haliwahusu wafanyakazi wa kampuni na familia
zao tu bali kwa jamii nzima kwa kuwa wafanyakazi wa TBL Group ni sehemu
ya jamii na wanaishi kwenye jamii.
“Sera za kampuni yetu zinahimiza
kulipa kipaumbele mkubwa suala la Usalama na afya sio kwa wafanyakazi tu
bali usalama wa jamii nzima na ndio maana kampuni imekuwa mstari wa
mbele kufadhili na kushiriki katika kampeni mbalimbali za usalama na
miradi ya Afya na Mazingira”.Alisema Marco.
Kuhusiana na ufadhili wa semina
ya wakaguzi wa magari kutoka Jeshi la polisi na walimu wa shule za
msingi na ekondari alisema kuwa kampuni imekuwa ikifanya kazi kwa karibu
na taasisi hizo kuhusiana na masuala ya usalama hususani kampeni za
usalama barabarani lengo kubwa likiwa ni kupunguza matukio ya ajali
nchini.
Moja ya lengo lengo letu
tunalotekeleza ni kuhamasisha unywaji wa kistaarabu kwa jamii hivyo kama
kampuni inayotengeneza vinywaji tunalo jukumu la kuelimisha masuala ya
usalama kwa ujumla na tunaamini Jeshi la polisi kama msimamizi wa
masuala ya usalama barabarani nchini linapaswa kuungwa mkono na kupewa
ushirikiano mkubwa kuhakikisha linafanikisha kufikisha elimu ya usalama
na usalama barabarani kwa wananchi wengi.
Kwa upande wa walimu na wanafunzi
alisema kuwa kampuni itaendelea kushirikiana nao ikiwemo wadau wengine
kuhakikisha wanapata elimu ya usalama barabarani “Ukifundisha walimu
ni rahisi elimu hii kuwafikia wengi na wanafunzi wakipata elimu ya awali
ya masuala ya usalama na usalama barabarani wanakua wakiwa na uelewa
mpana wa kujikinga na kuchukua tahadhari.
Alisema suala la kuelimisha jamii
kuhusiana na usalama barabarani ni jambo ambalo kampuni ya TBL Group
itaendelea kulivalia njuga kwa nguvu zote kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi na wadau wengine
0 maoni:
Chapisha Maoni