Jumatatu, 25 Julai 2016

WABUNGE CHADEMA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI


Jeshi la polisi mkoani Arusha, limewaita kwa mahojiano, mbunge wa Karatu,Wilbroad Qambalo, mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso na Mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu,Jubilate Mnyenye kutokana na kupuuza agizo la kutofanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.

Mwingine ambaye ametakiwa kwenda kuripoti polisi ni Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Karatu, Lazaro Bajuta.

Wakizungumza jana baada ya kukabidhiwa barua za wito wa polisi, Qambalo na Paresso walisema wamestuka kutakiwa kuripoti ofisi ofisi ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Arusha jumatano.

Parreso alisema,walipokea barua jana saa sita mchana na kutakiwa kuripoti kwa RCO, saa nane  lakini wakampigia na kumweleza wana ratiba nyingine tayari waende jumatano na akakubali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkombo alipotakiwa kuelezea agizo hilo alisema yupo likizo.

0 maoni:

Chapisha Maoni