Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine
ameziasa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) kutimiza masharti ya kupata vibali vya kuishi na
kufanya kazi Tanzania kwa Wataalamu wa kigeni wakiwamo makocha,
madaktari na wachezaji kabla ya kuingia kandarasi.
Masharti hayo
ni vibali vya kufanya kazi nchini, visa ya kuishi nchini, vibali vya
kucheza mpira wa miguu nchini, vibali vya kufundisha mpira na vibali vya
watalaamu wengine kama madaktari na hayo ni kwa mujibu wa Idara ya
Uhamiaji na Serikali, lakini wakati huohuo kwa wachezaji nao kukatiwa
leseni ya kucheza kutoka TFF.
“Mchezaji au
mtaalamu ye yote anapokuja nchini na kuanza mazoezi na timu yo yote
anachukuliwa yuko kazini. Tusingependa watu wapate usumbufu. Kama Katibu
Mkuu nimepata taarifa kutoka mamlaka zinazohusika kuwa nifuatiulie kuwa
kuwa sisi ndio waratibu soka nchini, natakiwa kufuatilia,” amesema
Selestine.
“Vilabu
vihakikishe vyeti vya taaluma vinawasilishwa TFF kwa ajili ya ukaguzi
kabla ya kutiliana kandarasi na wachezaji au walimu. Inawezekana
hawahitajiki. Ni vema wakafanya uratatibu wa kuhakiki,” amesema.
Wakati huohuo,
huo huo TFF imeagiza klabu kuendelea na usajili kabla ya Agosti 6, 2016
ambayo itakuwa siku ya mwisho na kwamba hakutakuwa na muda wa kuongezwa
kwa klabu ambayo itashindwa kukamilisha usajili kwa wakati.
0 maoni:
Chapisha Maoni