Postedy by Esta Malibiche on July 22, 2016 in JAMII with No comments
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro,
akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana alipokuwa akitoa taarifa
ya matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa
silaha.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro,
akiwaonesha waandishi wa habari bunduki aina ya gobore walioikamata
kabla ya kutumika kwa ujambazi wakati akitoa taarifa ya matukio
mbalimbali ya uharifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha mkoani
humo leo mchana.
Kamanda
Sirro akionesha simu walizokutwa nazo watu wanaodaiwa vinara wa kupora
simu kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jijini.
Wapiga picha za vituo mbalimbali vya televisheni wakichukua taarifa hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………………………………………….
……………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa
kuliingia mapato taifa ya sh.milioni 198 kutokana na zoezi la uhakiki wa silaha lililofanyika mapema mwaka huu.
Jeshi
hilo limefanikiwa kuhakiki jumla ya silaha 14,107 kwa kipindi cha
kuanzia Machi Mosi hadi Juni 30 mwaka huu, vile vile Jeshi hilo
limefanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa sugu 1,065.
Hayo
yameelezwa leo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
Simon Sirro wakati akitoa taarifa za matukio mbalimbali ya uhalifu
pamoja na zoezi la kuhakiki wa silaha hizo.
Alisema zoezi la uhakiki wa silaha lilihusisha mikoa ya kipolisi ya Temeke, Ilala na Kinondoni.
“Idadi
ya watu waliojitokeza kuhakiki silaha kwa mikoa yote ni 11,602, na
silaha zilizohakikiwa ni pistol 5,073, shotgun 4,707 na rifle 2,974,”
alisema.
Kamishna
Sirro alisema dosari ndogo ndogo zilizojitokeza katika zoezi hilo ni
kama vile wamiliki wa silaha kuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 70, na
wengine kumili silaha za marehemu kinyume na taratibu.
“Hawa
kwa kweli hatukuwaruhusu waendelee kumiliki hizo silaha, hivyo tulibaki
nazo na wale walioshindwa kuzilipia silaha zao kwa muda mrefu pia
tulibaki nazo,” alisema.
Kamishna
Sirro alisema kutokana na sababu hizo jumla ya silaha 66 walibaki nazo
(kusalimishwa), ikiwa ni shotgun 36, rifle 10 na pistol 20.
Katika
operesheni maalumu iliyowezesha kukumata watuhumiwa sugu 1,065,
Kamishna Sirro alisema watuhumiwa hawo walikatwa kwa makosa mbali mbali
yakiwemo ya makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu.
“katika
hawa tumefakiwa kuwakamata watengenezaji wa pombe haramu ya gongo
wakiwa na lita 952 pamoja na mitambo mitatu, vile vile kuna wavutaji wa
bangi na puli zao 277.
“Matukio mengine ni pamoja na kukamatwa kwa kete 210, misokoto 144, pamoja na wacheza kamari,” alisema.
Katika
hatua nyingine Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu
kwa makosa ya uporaji wa simu katika maeneo mbali mbali ya kinondoni,
mtuhumiwa wa kwanza ni Richard Augustino 18 aliyekamatwa Julai 11 mwaka
huu maeneo ya Coco Beach akiwa na sumsung yenye thamani ya sh. 500,000.
“Wengine
ni Abdalah Chande 36 aliyekematwa Julai 11 mwaka huu maeneo ya Magomeni
Mapipa akiwa na simu 11 za wizi, na Abdalah Saidi 22 ambaye alikamatwa
maeneo ya Mapipa julai 14 mwaka huu akiwa na pikipiki aina ya boxer
ambayo ilikuwa ikitumika katika matukio ya ukuporaji simu,” alisema.
0 maoni:
Chapisha Maoni