Ijumaa, 22 Julai 2016

DC KASESELA AFUNGUA KONGAMANO LA KUJADILI MAENDELEO NA MATUMIZI YA RASILIMALI

 Postedy by Esta Malibiche on July 22

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wanafunzi walioshiriki kongamano 



Mkuu wa wilaya akipokea kitabu toka kwa bwana Daniel El Noshokaty ambaye alikabidhi vitabu kwa kila mwananfunzi kwa ajili ya kujisome


wanafunzi  wakimskiliza Mkuu wa wilaya


Wanafunzi walioshiriki kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya Kasesela pamoja na Daniel Noshokaty ambae ni mwakilishi wa shirika la  KAS

MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefungua kongamano la kujadili Maendeleo na matumizi ya rasilimali watu,lililowahusisha Wanafunzi wa shule za sekondari.
  Kongamano lilifanyika katika chuo kikuu huria kilichopo mkoani Iringa na kuhudhuriwa na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Lugalo, St Joseph, Kleruu, Kwelu, Highland na Mkwawa.
 Kongamano hilo liliandaliwa na umoja wa walimu wa masomo ya Uraia CETA wakishirikiana na taasisi ya kijeruman KAS.kongamano hilo ilililokuwa na mada zenye kutambua uwezo wa nchi katika kuleta thamani kwa rasilimali zilizopo Tanzania hasusan katika Mkoa wa Iringa 
 . Katika hotuba yake mkuu wa wilaya alisistiza kuwa rasilimali kubwa inayotakiwa kufanyiwa kazi ni Binadamu. 
Ksasesela alisema binadamu akijengewa uwezo anaweza kubadilisha rasilimali hizi ziwe na faida kwa maisha yake na wengine.
  Alisistiza suala la nidhamu kama msingi wa maisha, upendo na udailifu vinalete mabadiliko katika maisha ya mwanadamu.
 Naye Mwakilishi wa KAS bwana Daniel El Noshokaty awali akimkaribisha Mkuu wa wilaya alisema Taasisi ya KAS imeanza toka mwaka 1964 ikiwa na kazi ya kuelimisha wananchi juu ya elimu ya uraia hapa Tanzania na imetoa vitabu vingi kuhakikisha watanzania wanapata uelewa wa elimu hiyo. 
 Noshokaty alisema Kwa Mkoa wa Iringa wataendelea kuelimisha wanafunzi watambue fursa zilizopo katika rasilimali nyingi. 

0 maoni:

Chapisha Maoni