Ijumaa, 22 Julai 2016

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI ATEMBELEA CHUO CHA USAFIRISHAJI

01Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipotembelea Chuo hicho kukagua miundombinu yake.
02Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa kuhusu namna nzuri ya kukiwezesha Chuo hicho kujiendesha kwa faida na kuboresha miundombinu yake.
03Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi wa anga katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT Eng. Azizi Mdimi akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani injini ya ndege inayotumia kwa mafunzo wakati alipokagua Hanga katika chuo hicho.
04Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua ndege inayotumiwa kufundishia wanafunzi wanaosomea utengenezaji wa ndege na urubani alipotembelea Chuo cha Usafirishaji NIT.
05Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa akimuonesha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani moja ya kitabu kinachotumiwa kufundishia marubani na wahandisi wa ndege alipotembelea maktaba ya chuo hicho.
06Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mtambo unaopima magari ili kujua ubora wake kabla ya kuanza kutumika hapa nchini alipotembelea Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT.
(Picha na Benjamin Sawe-Maelezo)

0 maoni:

Chapisha Maoni