Balozi wa kujitolea katika kuhamasisha usafi wa mazingira, Omary Kombe Jumamosi ya  Julai 30.2016 anatarajia kuungana na wananchi mbalimbali wa Kigamboni katika zoezi la ufanyaji usafi katika fukwe ya  Feri-Mnazi Kinda  mpaka chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Magogoni na jirani na Jeshi la Navy.
Kwa mujibu wa Balozi huyo, amebainisha kuwa siku hiyo wananchi mbalimbali wameombwa kujitokeza wakiwa na vifaa vyao vya kufanyia usafi na kuungana kwa pamoja katika ufanyaji wa usafi wa mazingira.
“Jumamosi ya Julai 30.  Ni siku maalum ya usafi wa mazingira yetu. Hivyo tutafanya usafi  katika fukwe za Feri  kwani tayari fukwe hizi zimeharibika vibaya kutokana na uchafu. Watu wamegeuza  bahari kuwa dampo, kitu ambacho sio sahihi zoezi hili lina wahusu wadau wote kutoka ndani ya Wilaya yetu mpya ya Kigamboni na Mkoa kwa ujumla.” Alieleza Bwana Kombe.
Aidha, aliongeza kuwa, kuunga mkono juhudi za Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha mazingira yanakuwa safi, amewaomba wananachi kujitokeza kwa wingi katika kushiriki zoezo hilo ambapo pia kutakuwa na harambee yenye lengo la kukusanya fedha za kujenga choo  katika maeneo hayo ya Feri.
“Zoezi hili la usafi litakuwa ni  kubwa na endelevu. Pia kutakuwa na Harambee ya kuchangisha fedha ambazo tutajenga Choo eneo la feri. Kwa sasa hakuna choo na wavuvi na watu wa maeneo yale kwani wamekuwa na tabia ya baadhi yao kujisaidia pembeni mwa bahari kitu ambacho sio sahihi kwani kinaweza kupelekea magonjwa wa milipuko/maambukizi.
Tuungane kwa pamoja na Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bwana Paul Makonda, Meya wa Jiji na wadau wengine mbalimbali kuliweka jiji letu katika hali ya usafi” alimalizia Bwana Kombe.
Mbali na tukio hilo la usafi. Pia Bwana Omary Kombe anatarajia kutoa tuzo maalum ya mazingira kwa Kamanda wa Jeshi la Navy, kutokana na kujali kwao usafi wa Mazingira.
DSC_0446Balozi wa kujitolea katika kuhamasisha usafi wa mazingira, Omary Kombe (kushoto) akitoa moja ya vifaa vya usafi katika shughuli za kuhamasisha usafi katika Jiji la Dar es Salaam.