Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Ilangali Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma jana
muda mfupi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika zahanati ya kijiji
hicho. Mradi huo wa zahanati umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA Tsh.
Milioni 25, Mbunge wa Jimbo la Mtera (Livingstone Lusinde) Tsh. Milioni
14.3 na Wananchi wa kjiji hicho Tsh. Milioni 12.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akizindua
mradi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Maila iliyopo
Chamwino, Dodoma jana, mradi huo umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA
kupitia Mradi wa Ujirani Mwema, Tsh. Milioni 115.83 na Wananchi wa Kata
ya Manda Tsh. Milioni 33.72. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mtera,
Lingstone Lusinde.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akimkabidhi
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga (kulia) Hati ya Makabidhiano
ya mradi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Maila iliyopo
Chamwino, Dodoma jana, mradi huo umefadhiliwa kwa ushirikiano wa TANAPA
kupitia Mradi wa Ujirani Mwema, Tsh. Milioni 115.83 na Wananchi wa Kata
ya Manda Tsh. Milioni 33.72. Watano kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
TANAPA, Witness Shoo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Tanzania – TANAPA ambaye pia
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Shirika hilo, Witness Shoo akitoa
taarifa ya juu ya miradi miwili iliyofadhiliwa na Shirika hilo katika
vijiji vya Ilangali na Manda. Alisema shirika hilo limechangia Tsh. Milioni 148.3 kupitia mradi wa Ujirani Mwema.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia)
akikagua vitanda vya mradi wa bweni la wasichana wa shule ya Sekondari
Maila iliyopo Chamwino, Dodoma jana, mradi huo umefadhiliwa kwa
ushirikiano wa TANAPA kupitia Mradi wa Ujirani Mwema, Tsh. Milioni
115.83 na Wananchi wa Kata ya Manda Tsh. Milioni 33.72. Kulia ni Mbunge
wa Jimbo la Mtera, Lingstone Lusinde na Mwenyekiti, Halmashauri ya
Wilaya ya Chamwino, Samuel Amon (wa tatu kulia).
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa tatu kulia)
akiongoza msafara kukagua fensi ya bweni la wasichana katika shule ya
Sekondari Maila muda mfupi kabla ya kuzinduliwa. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Witness Shoo na Mbunge wa Jimbo la Mtera,
Livingstone Lusinde (wanne kulia)
Picha ya pamoja.
Taswira ya jengo la Zahanati ya kijiji cha Ilangali lililofadhiliwa na TANAPA.
Taswira ya jengo la Bweni la Wasichana shule ya Sekondari Maila lililofadhiliwa na TANAPA.
Na Hamza Temba – WMU
____________________________________
Serikali
kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepanga kulipatia ufumbuzi
tatizo la uvamizi wa Wanyamapori kwenye makazi ya watu wanaozunguka
Hifadhi zenye Wanyamapori nchini kwa kuwashirikisha wananchi wa vijiji
hivyo, kuwapatia mafunzo na silaha maalum za kujilinda na kufukuza
wanyamapori hao wakati wa dharua.
Hayo
yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Ramo Makani
akizungumza na wananchi wa vijiji vya Manda na Ilangali Wilayani
Chamwino Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi na
uzinduzi wa miradi iliyofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA) kupitia Mradi wa Ujirani Mwema katika vijiji hivyo.
Akijibu
kero iliyowasilishwa kwake na Mbunge wa Jimbo la Mtera, Livingstone
Lusinge katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye vijiji hivyo kuhusu
Wanyamapori wanaovamia maeneo ya vijiji vya jirani na Hifadhi ya Ruaha
na kuharibu mazao ya wananchi, Eng. Makani alisema, changamoto hiyo
inashuulikiwa kwa upana wake na kwamba Serikali inakuja na mpango wa
kukabiliana nayo kwa kuwashirikisha wananchi wa vijiji husika.
Akizungumzia
mpango huo alisema kuwa Serikali itaanzisha mafunzo maalum ya kujikinga
na Wanyamapori kwa baadhi ya wananchi watakaoainishwa kwenye maeneo
husika na kupewa silaha maalum kwa ajili ya kuwafukuza kabla ya kuleta
madhara. Aliongeza kuwa Askari wa Wanyamapori waliopo pamoja na
changamoto za kijiografia za baadhi ya maeneo hawatoshi kulinda maeneo
yote ya vijijini hususani wakati wa dharua hivyo kwa kuwapa mafunzo na
zana na kujilinda baadhi ya wananchi itasaidia katika kukabilina na
tatizo hilo kwa wakati.
Katika
hatua za maandalizi ya awali ya mpango huo, aliwaagiza viongozi wa
vijiji vya Ilangali na Manda ambavyo vinayozunguka Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha kuanza kazi ya kutambua vijana wakakamavu, wenye elimu, uadilifu,
uaminifu na maadili bora kuanzia watano hadi kumi kwa ajili ya kujiunga
na mpango huo pale utakapokuwa tayari kuingia kwenye hatua ya
utekelezaji.
Hapo
awali akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa zahanati ya kijiji cha
Ilangali na baadae kuzindua mradi wa bweni la wasichana shule ya
Sekondari Maila iliyofadhiliwa na TANAPA, kwa niaba ya Waziri wa
Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, Naibu Waziri, Eng. Makani
alisema kuwa misaada hiyo ni sehemu faida za uhifadhi ambayo wananchi
wananufaika nayo kwa kushirikiana na Serikali katika uhifadhi. Aliwataka
wananchi hao kuendelea kushirikiana na Serikali katika uhifadhi ili
faida kama hizo ziendelee kupatikana kwa wingi kwa kuwa uhifadhi
ukiimarika na wanyamapori wakaongezeka na utalii nao utakua na kuongeza
mapato zaidi.
“Fedha
zilizotumika katika Mradi huu tunaoushuhudia hapa leo ni sehemu ya
faida za Uhifadhi, tunawaomba sana wananchi muendelee kuunga mkono
juhudi za Serikali za kulinda Wanyamapori na kupiga vita ujangili,
tuendelee kulinda chanzo cha fedha hizo, tukipata watalii wengi zaidi na
fedha hizo zitaongezeka maradufu. Alisema Makani.
Akizungumzia
miradi hiyo miwili, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa
Shirika hilo, Witness Shoo alisema kuwa shirika hilo limechangia Tsh. Milioni 148.3 katika
miradi hiyo ya Ujirani Mwema. Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka
1994 – 95 na 2014 – 15 Shirika hilo limechangia jumla ya Tsh. Bilioni 2
kwa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha katika miradi ya
sekta ya ya elimu, maji, afya na uhifadhi kwa ujumla.
0 maoni:
Chapisha Maoni