Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul
(wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,
wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi
dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Wengine ni maofisa mbalimbali wa
chama hicho.
Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Shaweji Mketo, akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam , wakati wa kutoa msimamo wa chama
hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa
cha Cuf. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi Taifa, Mustafa Wandu na
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed
Mazrul.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI
wa Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF) Shaweji Mketo amesema iwapo
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ataendelea kukifuatilia
chama hicho wanachama wa chama hicho watekwenda ofisini kwake
kumsalimia.
Mketo
ameyasema hayo Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni leo Dar es Salaam
leo wakati Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar,
Nassor Ahmed Mazrul alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi
ya vyama vya siasa hasa cha Cuf.
“Tunasema
sisi Cuf hatumuogopi IGP na kama ataendelea kutufuatafuata haita pita
wiki mbili tutamfuata kwenda kumsalimia ofisi kwake” alisema Mketo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul
alisema
chama hicho kimesikitishwa na kauli ya IGP aliyoitoa hivi karibuni
wakati akihojiwa Tido Mhando wa Kituo cha Televisheni cha Azzam kuwa
jeshi hilo wakati wowote litamkamata Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim
Seif Sharif Hamad kwa kuwachochea wafuasi wake ili waichukie serikali
iliyopo madarakani.
Alisema
baada ya kuitafakari kauli hiyo ya IGP wamebaini kwamba hivi sasa IGP
Mangu ameamua kuwathibitishia watanzania kuwa jeshi la polisi ni idara
maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mazrul
alisema kwa muda mrefu IGP Mangu amekuwa akilitumia jeshi la polisi
kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuhujumu demokrasia na kukiuka
haki za binadamu kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kutokana na anguko kubwa la kukataliwa na wananchi kama ilivyothibitika
kabnla na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.
Alisema
jeshi la polisi limekuwa na utaratibu wa kukamata raia, kuwapiga
kuwabambikia kesi, kuwashikilia na kuwatesa katika vituo vya polisi bila
ya kuwafikisha mahakamani.
Mazrul alisema hadi sasa zaidi ya wananchi 400 wameathiriwa kutokana na hujuma za jeshi la polisi kwa kuwabambikia kesi.
0 maoni:
Chapisha Maoni