Mratibu wa Mradi wa Usalama Barabarani kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), Marry Kessy.
Mratibu wa Mradi wa Usalama Barabarani kutoka Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) , Marry Kessy akitoa elimu kwa waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani jijini Dar es Salaam, ambapo waandishi wa habari walipata kujifunza mambo yanayohusu usalama wa barabarani ikiwepo kupewa ripoti ya ajali ambazo hutokea duniani na Tanzania, umuhimu wa uvaaji kinga (helment), umuhimu wa uvaaji mkanda kwenye gari, madhara ya ulevi uendeshapo chombo cha moto na vizuizi kwa watoto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi, ASP Masoko akitoa mada kuhusiana na sheria ya usalama barabarani ya Tanzania inavyofanya kazi, wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa Usalama wa Barabarani waShirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) , Callie Long akitoa elimu kwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku moja jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari mbalimbali waliohudhuria mafunzo ya usalama barabarani ya siku moja jijini Dar es Salaam ambapo walipata kujifunza mambo yanayohusu usalama wa barabarani ikiwepo kupewa ripoti ya ajali ambazo hutokea duniani na Tanzania, umuhimu wa uvaaji kinga (helment), umuhimu wa uvaaji mkanda kwenye gari uendeshaji vyombo vya moto na vizuizi kwa watoto
0 maoni:
Chapisha Maoni