Alhamisi, 28 Julai 2016

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI WILAYANI LUDEWA MATATANI KWA KUBAKA WANAFUNZI WAKE .......

Esta Malibiche on July 28


MWALIMU Abute Fungo (40 ) wa shule ya msingi Kimelembe kata ya Nkomang’ombe Ludewa mkoani Njombe pichani  atiwa mikononi mwa polisi Ludewa kwa tuhuma za kubaka na  kuwapiga picha sehemu za siri wanafunzi wake  zaidi wanne  na  kuwalipa kati ya Tsh 500  na  1000
“Mwalimu amenilazimisha kufanya nae mapenzi  zaidi ya mara nane na alikuwa akinilazimisha kumeza dawa za majira akiniambia kuwa zinazuia mimba hata hivyo nilikuwa nameza bila kutumia maji”.alisema mtoto mmoja wa  watoto  hao

Watoto  hao  walisema  kuwa mwalimu  wao  huyo alikuwa akiwafanyia  vitendo  hivyo kwa nyakati tofauti  katika vichaka vilivyopo jirani na  kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania katika kijiji cha Kimelembe Kata ya Mkomang’ombe.
Wakizungumza mtandao huu  wa  matukiodaimaBlog  watoto wanne walioamua kutoa ushuhuda wao kabla na baada ya kufika polisi walisema mwalimu amekuwa akitenda unyama kwa  wanafunzi kila mwaka na kuongeza kuwa wenzao zaidi ya nane walishabakwa kwa kipindi cha mwaka jana na wazazi wachache kulipana nje ya mahakama.

Watoto hao wenye umri chini ya miaka 14 waliongeza kuwa mwalimu alikuwa akiwalipa pesa kati ya sh500 hadi 1000 kama malipo kabla na baada ya kufanya kitendo hicho polini.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Pudenciana Protas amekiri kukamatwa kwa mwalimu huyo na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa. 
Watoto hao ambao ni wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Kimelembe wilayani hapa walisema kuwa ubakazi huo umefanya kwa muda mrefu na mwalimu huyo lakini wamekuwa wakishindwa kutoa taarifa kwa wazazi wao na walimu wengine kutokana na kuogopa vitisho kutoka kwa mwalimu huyo.
Walisema kuwa mwalimu huyo amekuwa akitoa adhabu kali kwa mwanafunzi anayekataa kufanya naye tendo hilo hiyo imekuwa inawapa wakati mgumu wanafunzi kukataa kufanya hivyo wakihofia kuzalilishwa kwa adhabu kali mbele ya wanafunzi wengine.
Wanafunzi hao walisema kuwa walianza kuitoa siri hiyo kwa mama yao mdogo wakati wakifua nguo za shule katika mto nchuchuma ndipo mama yao mdogo huyo alipoamua kuwaeleza wazazi wao na kuchukua uamuzi wa kulipeleka jambo hilo katika Serikali ya Kijiji.
Walisema baada ya uongozi wa kijiji kupata taarifa hiyo ndipo wakaamua kutoa taarifa katika jeshi la Polisi ambapo jeshi la polisi liliamuru kukamatwa kwa mwalimu huyo na kufikishwa Mahakamani.

0 maoni:

Chapisha Maoni