Jumatatu, 25 Julai 2016

ALICHOSEMA ZITTO KABWE BAADA YA MAGUFULI KUCHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CCM TAIFA

Postedy by Esta Malibiche on July 26 in SIASA with No comment

Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Zitto Kabwe.

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia account yake ya facebook amempongeza Rais Dkt.John Pombe Magufuli kukabidhiwa uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kupata  kura zote  za ndio 2398.
Huu ndio ujumbe wake,
“Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda.
“Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.
“Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais.” –Zitto Kabwe

0 maoni:

Chapisha Maoni