Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Dkt. Abdallah Possi akionyesha Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Utumikishwaji wa Watoto Tanzania wa Mwaka 2014. Uzinduzi huu umefanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.
………………………………………………………………………………………..
Benjamin Sawe-Maelezo.
Utumikishwaji wa watoto umekuwa ni tatizo kubwa duniani ambapo kutokana na tawkimu za makadirio za mwaka 2000-2012 za Shirika la Kazi Duniani asilimia 11 (watoto milioni 264) ya watoto wote duniani wenye umri wa miaka 5-17 wnatumikisahwa kwenye ajira za aina mbalimbali sawa na asilimia 11 ya watoto wenye umri huo.
Kwa upande wa Tanzania, utumikishwaji wa watoto kwa mwaka 2014/15 matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kati ya watoto milioni 15 wenye umri kati ya miaka 5 hadi 17 (watoto milioni 4.2) sawa na asilimia 28.8 wanatumikishwa katika kazi mbalimbali
Takwimu hizo zinaonesha kuwa sekta za kilimo na uvuvi zimeendelea kuwa sekta zinazoajiri watoto wengi zaidi ikiwa ni kiwango cha asilimia 92.1 ya watoto wote wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi na wengi wao wanaishi vijijini.
Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya matokeo ya utafiti wa utumikishwaji wa watoto Tanzania Bara wa mwaka 2014, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa anasema matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa watoto hutumia zaidi ya nusu ya muda wao wa siku ikiwa ni asilimia 58.8 kwa shughuli za kujihudumia na usafi huku wasichana wakionekana kutumia muda mrefu zaidi kwa shughuli hizo kwa kiwango cha asilimia 58.3.
0 maoni:
Chapisha Maoni