Jumatatu, 18 Julai 2016

RC Makonda afanya uzinduzi wa NAS-DAR AIRCO nchini, kwa kuanza watanzania 60 wapata ajira



Katika kipindi ambacho Tanzania inaendelea kukua kwa kasi kiuchumi na hivyo kuwepo kwa wageni wengi ambao wamekuwa wakiwasili nchini, kampuni ya Mwanza Ground Handling Company (AIRCO) imeungana na kampuni nyingine ya National Aviation Services (NAS) ili kutoa huduma katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa kuboresha huduma zinazotumia usafiri wa anga kwa kuhudumia abiria, ndege na shughuli za mizigo.


Akizungumzia ushirikiano huo ambao umewezesha kupatikana kampuni ya NAS-DAR AIRCO, Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO, Salim Ajib alisema NAS na AIRCO zimeungana kwa pamoja ili kuboresha huduma ambazo zinatolewa kwa abiria ambao wanatumia usafiri wa ndege.

Alisema wamejipanga kutoa huduma bora ambazo zitaisaidia Tanzania kupokea wageni wengi zaidi ambao kwa namna moja au nyingine itasaidia kukuza uchumi wa nchi lakini pamoja na hilo ushirikiano huo umekuja na neema kwa watanzania kwa kupata ajira na ambapo kwa kuanza wameajiri wafanyakazi 60.

Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO, Salim Ajib akizungumza kuhusu kampuni ya NAS-DAR AIRCO ambayo itakuwa ikifanya kazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. (Picha zote na Rabi Hume, Mo Blog)

"Tunajua kuna changamoto na sisi tupo tayari kuingia katika ushindani huo kwa kuwapa wateja huduma bora ... tunafahamu Tanzania inakua kwa sasa na huduma zetu tunatumai kusaidia ukuaji wa uchumi kupitia huduma zetu wa abiria wanaotumia uwanja wa Mwalimu Nyerere,

"Tumetoa nafasi za kazi kwa watu 60 na tumewapa mafunzo kwa ajili ya kuanza kazi hivi karibuni na baadae tutaongeza wengine sababu tutakuwa na huduma nyingi ambazo tutakuwa tunazitoa," alisema Ajib.


Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampuni ya NAS-DAR AIRCO, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiikaribisha kampuni hiyo katika mkoa wake kwa ajili ya kutoa huduma kwa abiria wa usafiri wa anga.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika halfa hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwakaribisha NAS-DAR AIRCO kutoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere na kutoa angalizo kwa kampuni ya Swissport kuwa iwe makini kwa sababu sasa wamepata mshindani.

"Mji wetu bado unakua na tunazidi kuongezeka kama nyie mkitoa huduma nzuri hata wageni wataongezeka na wengine watakuja hata kuwekeza kabisa niwakaribishe nchini lakini pia nitume salamu kwa Swissport kama walikuwa wanafanya kazi na kuna sehemu wanajikwaa sasa wamepata jirani," alisema Makonda.

Makonda alisema ujio wao wa kufanyakazi nchi uwe na mfumo mpya ili kuboresha huduma kwani kwa sasa kumekuwepo na taarifa za abiria wengine wanaofika nchini kupoteza mizigo yao na hivyo kuanza kupoteza imani kama kiwanja hicho kinakuwa salama kwa kukitumia pindi wanapowasili au kuondoka nchini.

Na Rabi Hume, Mo Blog

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya NAS-DAR AIRCO, David Handerson akielezea jinsi ambavyo kampuni yao imejipanga kutoa huduma bora nchini.



Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya NAS-DAR AIRCO wakionyesha mavazi ambayo watakuwa wakiyatumia muda wa kazi.











Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO wakifanya uzinduzi wa NAS-DAR AIRCO nchini.





Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mwenyekiti wa NAS-DAR AIRCO wakipongezana baada ya kufanya uzinduzi.

Mgeni rasmi,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NAS-DAR AIRCO.

Baadhi ya watu waliohudhuria halfa ya uzinduzi wa NAS-DAR AIRCO.







Bendi ikitoa burudani baada ya uzinduzi kufanyika.

0 maoni:

Chapisha Maoni