Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
imetoa hati ya kukamatwa kwa Meneja wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva ,Diamond
Platnumz, Hamis Tale ‘Babu Tale baada ya kutotii amri ya mahakama ya kulipa
shilingi milioni 250 katika kesi ya hati miliki.
Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na
Babu Tale kutotii amri ya mahakama iliyomtaka amlipe Shekhe Hamis Mbonde kiasi
hicho cha fedha.
Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo
kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza
nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume
na haki miliki.
0 maoni:
Chapisha Maoni