…………………………………………
Shirika lisilo la kiserikali la
Green Hope Organization lenye makao yake jijini Arusha leo imekabidhi
madawati 100 yaliotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa inayotokana na
mabaki ya chupa ya maji na mifuko ya plastiki
Akikabidhi madawati hayo kwa mkuu
wa mkoa Arusha Felex Ntibenda maarufu kwa jina la kijiko mkurugenzi
mtendaji wa kampuni hiyo Emmanuel Makongoro amesema madawati hayo
yametengenezwa kutokana na mabaki ya chupa tupu za maji na mifuko ya
plastiki
Amesema madawati hayo yatengenezwa
kutokana na agizo la Mh Rais John Pombe Magufuli , la kuhakikisha kuwa
hakuna watoto wanao kaa nchini kutokana na ukosefu wa madawati
Amesema gharama ya dawati moja ni
sh.80,000, ambapo wanakusudia kutengeneza madawati 3000 ambayo
watakabidhi mkoa Arusha kwa lengo la kusambaza wilaya zake
Makongoro,amesema teknolojia hiyo
ya kutengeneza madawati na meza kwa kutumia mabaki ya chupa tupu na
plastiki inakusudia kutoa ajira kwa vijana ambao watakuwa wakiuza chupa
hizo kwa sh.1500 kwa kila kilomoja.
Ameongeza kuwa wako kwenye mikakati ya kufungua vituo vya ukusanyaji wa chupa hizo kwenye jiji la Arusha
Amesema shirika hilo linatekeleza
mradi huo wa madawati kutokana na ufadhili wa shirika la misaada la
Canada (cida)Amesema shirika hilo limefungua ofisi jijini Mwanza kwa
ajili ya kukusanyia chupa na mifuko ya plasiti kwa ajili ya mradi huo wa
kutengeneza madawati.
Akipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa
wa Arusha Daudi Felex Ntibenda amelipongeza shirika hilo kwa msaada huo
wa madawati na kuomba wananchi wengine na taasisi mbali mbali kusadia
vifaa mbali mbali vya elimu.
Ntibenda, amezitaka taasisi
zingine za ufundi na mikoa mingene kuja Arusha kujifunza teknolojia hiyo
ya kutengeneza madawati na meza kwa kutumia mabaki ya chupa tupu za
maji na mifuko ya plastiki.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa
teknolojia hiyo itasaidia sana kupunguza uchafuzi wa mazingira pamoja na
kuongeza hajira kwa vijana wanao kusanya chupa tupu na kuuza kwa
taasisi hiyo
0 maoni:
Chapisha Maoni