Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi (Pichani juu kulia)
akizungumza na Mkurugenzi wa masuala ya Kidiplomasia katika Taasisi ya
Aga Khan, Balozi Arif Lalani alipotembelea Wizarani kwa ajili ya
kujitambulisha na kueleza nia ya Taasisi hiyo ya kuendelea kushirikiana
na Serikali ya Tanzania katika miradi ya maendeleo hususan katika sekta
ya elimu na afya.
Sehemu
ya wageni walioambatana na Balozi Lalani (hayupo pichani). Kulia ni
Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Aga Khan nchini, Bw. Amin Kurji nao
wakisikiliza mazungumzo kati ya Balozi Muombwa na Balozi Lalani (hawapo
pichani).
Balozi Lalani naye akizungumza na Balozi Mwinyi alipotembelea Wizarani.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Ramla Khamis
(kushoto), pamoja na Afisa Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika
Mashariki, Bi. Hellen Mgeta wakifuatilia mazungumzo.
Mazungumzo yakiendelea.
Balozi Mwinyi akiagana na Balozi Lalani na Bw. Kurji mara baada ya kumaliza mazungumzo.
0 maoni:
Chapisha Maoni