Jumatano, 27 Julai 2016

TANZANIA YAENDELEA KUPATA MAFANIKIO KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA WA VIKOPE (TRACHOMA).


Postedy by Esta Malibicheon July 27, 2016 in JAMII with No comments
VIKO1Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Neema Rusibamayila akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano uliowahusiaha  Wadau wa Wizara hiyo na washirika wa maendeleo Maendeleo kutoka Mfuko wa Malkia Elizabeth unaojihusisha na utokomezaji wa Ugonjwa wa Vikope na wale wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo (DFID).
VIKO3Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Malkia wa Uingereza unaojihusisha na utokomezaji wa ugonjwa wa Vikope katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania Dk. Aristid Bonifield akieleza namna Mfuko huo utavyoendelea  kuisaidia Tanzania kwa kuwa inafanya vizuri katika kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa nchini leo jijini Dar es salaam.
VIKO4Mkuu wa Idara ya Kimataifa ya Maendeleo nchini Tanzania (DFID) Vel Gnanendra akifafanua namna wadau wa maendeleo walivyojipanga kuiunga mkono Tanzania kwa kuhakikisha ugonjwa wa vikope (Trachoma) unatokomezwa nchini.
VIKO5Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele,   Upendo John Mwingira akizungumza wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
VIKO6Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sightsavers kutoka Uingereza Dk. Caroline Harper akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa kutokomeza ugonjwa wa Vikope leo jijini Dar es salaam.
VIKO7Washiriki wa Mkutano wa Kutokomeza Ugonjwa wa Vikope kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto  na Wale wa Mashirika ya Kimataifa wakiwa katika picha ya Pamoja leo jijini Dar es salaam.
Picha/Aron Msigwa – MAELEZO.
………………………………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
 Dar es salaam.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza kuwa licha ya Tanzania kuendelea kupata mafanikio katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Vikope (Trachoma) jamii bado inalojukumu la kuendelea kuzingatia na kufuata kanuni za afya kwa kufanya usafi wa mwili na mazingira ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano wa Wadau wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele,  Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Neema Rusibamayila amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza ugonjwa huo ikishirikiana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema kupitia idadi ya wagonjwa wanaougua vikope imeendelea kupungua mwaka hadi mwaka kupitia afua mbalimbali chini mpango ujulikanao kama “SAFEambao unahusisha huduma za Upasuaji,utoaji wa dawa za Antibayotiki, kuosha  pamoja na usafi wa mazingira
Ameongeza wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeweza kufanikisha upunguzaji wa ugonjwa huo kwa kutoa dawa/tiba kinga kwa wananchi katika maeneo yaliyoathirika ambapo amesema kufuatia utafiti uliofanyika mpaka sasa wilaya 22 ugonjwa huo umepungua sana kiasi cha wananchi wa maeneo hayo kutohitaji dawa za tiba kinga.

0 maoni:

Chapisha Maoni