Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Dkt. Vicent Mashinji amewataka vijana wa Bavicha kutokuwa
wazembe wakufikiria bali kujipanga kwa ajili ya kushika dola mwaka wa uchaguzi
mkuu 2020 huku akiwapatia kanuni za kushinda uchaguzi huo.
Amesema
chama chao kimejipanga kushika dola hivyo wao kama vijana wanatakiwa
kuhakikisha wanatekeleza majukumu ya kufanya uchaguzi na kuwatambua wanachama
hai, pia kuhakikisha vijana wanashiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa
katika nafasi mbali mbali na kushinda.
“Nataka
niwape majukumu matatu ambayo mkiyafanya hayo 2020 tutashinda nakutangazwa,
moja hakikisheni tunaingiza wanachama wapya na kuwahakiki walio hai, nendeni
2019 kwenye serikali za mitaa vijana mgombee na tupate viongozi ngazi ya chini
viijana wasomi, na tatu kwa mwaka huu kila kijana ajue nafasi zitakozogombewa
katika eneo lake hiyo itatusaidia kushinda nafasi nyingi za madiwani kwa
Tanzania bara na visiwani na haya ndiyo majukumu makubwa
ninayowapatia,” amesema Mashinji.
0 maoni:
Chapisha Maoni