Ofisa
Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa
Mauzo ya Nje (EPZA), Nakadongo Fares (kulia), akizungumza na waandishi
wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na
mamlaka hiyo. Kushoto ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge.
Meneja Uhamasishaji Uwekezaji, Grace Lemunge (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na wanahabari.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Star Infrastructure Development (T) Limited, Ananth
Bhat akizungumzia mradi wao wa uwekezaji uliopo mkoani Morogoro.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
———————————-
Na Dotto Mwaibale
MAMLAKA
ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) imeweza
kutengeneza ajira 36,000 kwa watanzania kupitia makampuni 140
yaliyowekeza hapa nchini.
Hayo
yamebainishwa na Ofisa Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka hiyo,
Nakadongo Fares Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka hiyo kwenye
maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016.
“Kupitia
makampuni 140 yaliyowekeza hapa nchini yameweza kutoa ajira kwa
watanzania 36,000 huku watoa huduma wakiwa 300,000” alisema Fares.
Alisema
kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuhasisha uwekezaji katika kanda maalumu
za kiuchumi, kuvutia na kuhamasisha uhuishaji wa teknolojia mpya,
kuhamasisha uwekezaji kwenye viwanda usindikikaji wa malighafi
zinazopatikana nchini, kutengeneza fursa za ajira na kuongeza pato la
fedha za kigeni nchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni