Jumatano, 27 Julai 2016

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MWIGULU NCHEMBA ATUA KATIKA MGODI WA NYAMHUNA UNAODAIWA KUUA MTANZANIA

Postedy by Esta Malibiche on July 27.2016 in News with No comment

 









Picha na Festo Sanga


Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba leo hii amewasili katika mkoa wa Geita  kwa ziara ya kikazi .
Waziri katika ziara yake amembelea  Mgodi wa Nyamhuna unaodaiwa kuwa, raia wa china ambao ni sehemu ya wamiliki wa mgodi huo wakishirikiana na watanzania walimtesa kinyama na kumjeruhi mmoja wa mtanzania mwenzetu aliyekuwa akifanya kazi katika mgodi huo uliopo Katoro-Geita.
 '''''''Imenilazimu kufika gereza la Geita kukutana na kijana huyo ambae yupo hai tofauti na taarifa za awali kuwa alifariki.Baada ya kujiridhisha kuanzia mavazi,majeraha,picha,sura na umbo lake kuwa ndiye kijana aliyeteswa vibaya na picha zake kusambaa mitandaoni na vyombo mbalimbali vya habari''''alisema Mwigulu
''''''Niliamua kwenda naye hadi mgodini lilipofanyika tukio hilo la kinyama,aliwatambua wahusika ambao walishiriki kufanya tukio hilo la kinyama  ambalo halikubarika hapa nchi''''''....alisema Mwigulu
Alisema  walioshiriki tukio hilo wanashikiliwa na jeshi la polisi, tayari kwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Aidha Waziri Mwigulu alisema amesikitishwa na kitendo hicho,kilichofanywa na waamiliki wa mgodi huo na kulaani vikali.Pia alisema ,serikali  ipo tayari kushirikiana  rai wema watakaofichua na kutoa taarifa popote pale zinazohusu  matukio au viashiria  vinavyohatarisha usalama  wa wananchi

"Usalama wetu,jukumu letu sote"





0 maoni:

Chapisha Maoni