Katika tukio la kuhuzunisha mtoto mmoja amepoteza maisha na mwingine mmoja kuathiriwa baada ya kufanyika uzembe katika hospitali ya Southwestern Sydney iliyopo katika jimbo la New South Wales, Australia.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Waziri wa Afya wa New South Wales, Julian Skinner alithibitisha kuwa ni kweli kumetokea tukio hilo na kutumia fursa hiyo kuomba radhi kwa niaba ya serikali ya jimbo hilo.
Alisema kuwa watoto hao waliozaliwa miezi miwili iliyopita walichanganyiwa mitungi ya gesi ya mitungi ya hewa ya kupumulia (Oxygen) na Nitrous Oxide na baada ya hapo mmoja alipoteza maisha na mwinginee kuathiriwa na gesi hiyo.
“Ni kweli tuki limetokea siku ya Alhamisi na nitumie nafasi hii kuomba radhi kwa familia zote ambazo watoto walio wameathirika na tukio hilo,
“Wizara ya Afya ya NSW ipo pamoja nao na itaendelea kushirikiana na familia za watoto hawa kwa kila hatua,” alisema Waziri Skinner.