Msafara
wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya
miaka 17 ‘Serengeti Boys’, uliondoka jana alfajiri Dar es Salaam,
Tanzania imetua salama jijini Antananarivo, Madagascar kwa ajili kambi
ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kuwania nafasi ya
kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6,
2016.
Mchezo wa
marudiano utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam, ulioko
Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kwamba mshindi
atakuwa amejiwekea mazingira mazuri ya kuwania nafasi ya kufuzu fainali
za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani huko
Madagascar.
Mkuu wa
msafara akiwa ni Ayoub Shaibu Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Soka la Vijana, maofisa wengine waliosafiri na timu hiyo ni Kocha Mkuu,
Bakari Nyundo Shime maarufu zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi, Daktari wa
timu hiyo, Shecky Francis Mngazija na Mtunza Vifaa, Andrew Vanance
Andrew.
Pia yumo Juma
Kaseja Juma ambaye kwa muda amechukua nafasi ya makocha wasaidizi,
Sebastian Nkoma na Muharam Mohammed ‘Shilton’ wanaohudhuria kozi ya
makocha ngazi ya juu inayoratibiwa na CAF.
Nyota
waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, Kelvin
Deogratius Kayego na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana
Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson
Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick Vitalis
Nkosi.
Viungo ni
Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian
Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi Ada huku
washambuliaji wakiwa ni Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola
na Muhsin Malima Makame.
Serengeti Boys
inakwenda kucheza na Afrika Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli kwa
jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa. Mshindi wa
jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika Kusini, atacheza na timu mshindi
kati ya Namibia na Congo-Brazaville.
Hivi karibuni
Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki mashindano ya
vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth
Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu
katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki. Ilishika nafasi ya tutu
nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
0 maoni:
Chapisha Maoni