Jumatatu, 25 Julai 2016

JB, Mataluma, Kitime ndani ya igizo ya kuhamasisha Kilimo

j1Muigizaji nyota wa filamu nchini, Jacob Steven (JB) akiizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na igizo jipya lilijulikanalo kwa jina la Kumekucha ambalo imeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid). Katika igizo hilo, JB ametumia jina la Mzee Kidevu.
j2Muandishi wa ‘script’ ya igizo la Kumekucha,  Priscilla Mlay (kulia) akizungumza wakati wa utambulisho wa igizo la Kumekucha ambalo limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid).
j3Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi wa USAID, Randy Chester (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa igizo hilo la Kumekucha utawaamsha na kupata maendeleo,”
j4Mwanamuziki mkongwe nchini, John Kitime (wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa igizo la Kumekucha ambalo limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid). Kitime ndiye aliyeingiza muziki katika igizo hilo.
j5 j6 waigizaji wa igizo hilo.
………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Msanii nyota nchini wa filamu, Jacob ‘JB’ Steven ni miongoni mwa waigizaji  mbalimbali walioshiriki katika igizo la  Kumekucha ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujishughulisha na kilimo kutokana na uhaba wa soko la ajira.
Igizo hilo ambali pia ni mchezo wa redio (radio plays) limeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media For Development International (MFDI) chini ya udhamini wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (Usaid) ya ushauri wa Taasisi ya chakula na lishe (TFNC), Taasisi ya TAHA, ACDI VOCA – NAFAKA,  Land O Lakes, Rudi, Mwanzo Bora, The Rice Council of Tanzania, Technoserve, ANSAF (Non State Action Forum) na taasisi ya AMSHA.
Katika filamu hiyo, JB anatumia jina la Mzee Kidevu ambaye kazi yake kubwa ni kununua mazao kwa wakulima kwa bei ya ukandamizaji na kuwafanya wakulima hao kuendelea kuwa na maisha duni huku yeye akijinufaisha.
Akizungumza katika uzinduzi huo, JB alisema kuwa amefurahi sana kushiriki katika filamu hiyo ambayo inafundisha na kuhamasisha vijana kujihusisha zaidi na masuala ya kilimo na kuacha tabia ya kukimbilia mijini kama suluhisho lao la kutatua matatizo yao.
“Nimepanda kushiriki katika filamu na mchezo huu wa redio, umenipa mwanga mkubwa na kupanua wigo wa kazi yangu ya kuigiza, kabla ya kuingia kwenye kuigiza, nilikuwa mnunuzi wa mazao hasa mahindi kule Kibaigwa na kusaga na kuuza unga wa chakula, hii ilikuwa fursa kwangu na nimeipenda, nawashukuru wahusika wote waliofanikisha filamu hii,” alisema JB.
Mkurugenzi wa masuala ya Uchumi wa USAID, Randy Chester alisema kuwa wamefurahi kujihusisha na masuala mbalimbali yaa maendeleo hapa nchini na kuamua kusaidia mradi huo ambao unahusika zaidi  maeneo ya  vijini.
“USAID imejihusisha katika miradi mingi ya maendeleo nchini, kama unajua, zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wanajihusisha na masuala ya kilimo, waahitaji kuendelezwa ili kufikia hatua kubwa ya maendeleo, mchezo wa Kumekucha utawaamsha na kupata maendeleo,” alisema Chester.

0 maoni:

Chapisha Maoni