Ilikuwa
moja kati ya Historia zilizotengenezwa katika wimbo wa ‘You and I’,
Taylor Kinney akicheza kama ‘Video Model’ katika kichupa cha nyimbo hiyo
iliyotoka July 2011 na kuwaweka kwa karibu wawili hao.
Gaga
(30) aliingia katika mahusiano ya kimapenzi na Kinney (35) rasmi kwa
kuthibitisha katika tuzo za Grammy mara baada ya kuchukua tuzo ya wimbo
bora wa PoP kwa mwaka huo kupitia kibao hiko hiko cha ‘You and I’ na
kuwa moja ya ‘Couple’ zilizovutia Zaidi nchini Marekani.
Kinney
anaeleza kuwa wakati wa kuchukua vipande vya video hiyo wote wawili
walikuwa na hisia kali sana na wakati mwingine walikuwa wakiharibu hata
baadhi ya maagizo ya Muongozaji video na kuchukua muda mrefu sana
kuikamilisha.
Gaga
ambaye amesainiwa na Label ya Def Jam pamoja na KonLive ambayo
inamilikiwa na Akon alivalishwa pete ya Uchumba na Kinney Februari 2015
na tayari walikuwa wamekwishaanza mipango ya ndoa mapema mwaka huu.
Mwanamuziki
huyo wa PoP pamoja na RnB nchini Marekani ameweka wazi kuvunjika kwa
uhusiano huyo hivi karibuni mara baada ya kupost picha katika mtandao wa
kijamii akiiwekea rangi nyeusi na nyeupe (black & white) na kueleza
kuwa yamekwisha kwa sasa na kila mmoja yupo mapumzikoni.
Gaga aliandika kuwa “Taylor
and I have always believed in soulmates, just like all couples we have
ups and downs and we have taking a break, we are both ambitious artist,
hoping to work through long distance and complicated schedules to
continue the simple love we have always shared. Please root us on. We’re
just like everybody else and we really love eache other”
Chanzo
kikubwa cha wawili hao kutengana bado hakijawekwa wazi kutokana na
wawili hao kufanya jambo hili kwa siri sana lakini inasemekana Kinney
alianza kuchepuka toka kipindi cha nyuma na hivyo kuleta hasira kali kwa
Gaga na kusababisha kuchukua maamuzi hayo yote.
Taylor
Kinney ambaye ni Raia wa Lancaster, Pennsylvania kwa sasa anatamba na
kipindi cha Televisheni cha ‘Chicago Fire’ huku akijishughulisha na
mambo mbalimbali ya Sanaa kama vile Mwanamitindo pamoja na uandaaji wa
filamu nchini Marekani.
Imeandaliwa na Derick Highiness
0 maoni:
Chapisha Maoni