Baada
ya kuwadatisha washabiki katika maonyesho mawili makubwa kule bayreuth
na tubingen sasa kamanda Ras Makunja anakipeleka kikosi kazi cha Ngoma
Africa band aka FFU-Ughaibuni katika onyesho kubwa la XXL Afro Summer
Jam mjini Stuttgart nchini ujerumani,onyesho hilo litafanyika siku ya
jumamosi 30 Julai 2016 katika ukumbi mkubwa Kulturhaus
Arena,uliopo Ulmer Str. 241, 70327 Stuttgart,ujerumani,akiongea
na vyombo vya habari kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda
Ras Makunja alisema Ngoma Africa band ni mali ya washabiki na ina kazi
moja tu nayo kudatisha washabiki katika kila onyesho bila kuremba remba ,
bendi hiyo iliyojizolea umaarufu na maelfu ya washabiki kila kona
duniani
imejiwekea rekodi ya aina yake kuwa ni bendi ya mwanzo ya
kiafrika kuimiri vishindo,na kudumu kwa miaka 23 ughaibuni na kufanikiwa
kuwanasa washabiki wa kimataifa.
ungana nao at www.ngoma-africa.com
|
|
|
|
|
|
0 maoni:
Chapisha Maoni