Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na
wajumbe hao wakati akifungua mkutano huo amesema kikao hicho kilikuwa
ni cha mwisho kwake kama mwenyekiti wa CCM , Akawashukuru wajumbe hao
kwa kumpa ushirikiano kwa miaka kumi yote akiwa Mwenyekiti na akaongeza
kwamba kama Chama cha Mapinduzi hakikupasuka mwaka jana hakiwezi
kupasuka tena kitaendelea kudumu na kudumu zaidi.
Amesema Kulikuwa na mafisi
yaliyokuwa yakingojea mkono udondoke tu ili yaweze kudaka na kula lakini
yaliambulia patupu chama kilisimama kidete na kuendelea na mipango
mizuri kwa ajili ya watanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mama Samia Suluhu, Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa
na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Rajab Luhwavi wakishiriki kuimba wimbo
maalum wa CCM kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
Msemaji wa CCM Ndugu Christopher
Ole Sendeka akisalimiana na Mzee Mark Mwandosya katikati ni Mjumbe wa
NEC kutoka mkoa wa Singida Ndugu Mwigulu Nchemba.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa NEC kutoka Zanzibar Ndugu Mohamed Abood akisalimiana na Mjumbe
mwenzake kutoka Zanzibar pia Balozi Ali Karume katikati anayecheka ni
Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Mzee Wilson Mukama.
Baadhi ya Wajembe wa NEC wakiwa kwenye mkutano huo kutoka kulia ni Mark Mwandosya, Profesa Peter Msola na Mzee Steven Waira.
Mpiga picha wa Makamu wa Rais Bw.
Adam Mzee kulia akiwaelekeza jambo waandishi wenzake kabla ya kuanza
kwa mkutano huo kutoka kushoto ni Emilian Malya kutoka Clouds Digital,
Bakari Kimwanga kutoka Mtanzania na Said Mwishehe kutoka Jambo leo.
Mjumbe wa NEC Godfrey Zambi akisalimiana na Mjumbe mwenzake Hussein Mwinyi katikati ni Khadija Aboud.
Christopher Olesendeka akibadilishana mawazo na wajumbe wenzake.
Baadhi ya wajumbe wakiwa tayari kwa mkutano huo
Wajumbe kutoka mkoa wa Pwani
Mzee Mark Mwandosya akizungumza na mjumbe mwenzake Peter Serukamba kutoka mkoani Kigoma
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya
Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa katikati akiwa na mkurugenzi wa Redio
Uhuru Angela Akilimali kulia na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uhuru
Selina Wilson wakiwa katika mkutano huo.
Wajumbe kutoka mkoani Mara wakiwa katika mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM kotoka Mkoa wa
Mwanza Bw. Joseph Kasheku Msukumu katikati akiwasikiliza wajumbe wenzake
Januari Makamba kulia na Said Mtanda wakati walipokuwa wakijadiliana
jambo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Ndugu Anthony Dialo akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa.
0 maoni:
Chapisha Maoni