Mkuu
wa vipindi wa Star TV, Yusuph Kamote kushoto akibadilishana mkataba na
Jay Msangi mara baada ya kusainiwa jijini leo. Akishuhudia tukio hilo
ni Chief Kiumbe
…………………………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Kituo cha Televisheni cha Star
Tv kimeingia makubaliano na kampuni ya Hall of Fame kwa ajili ya
kurusha moja kwa moja ‘live’ mapambano sita ya ngumi za kulipwa nchini
kuanzia mwezi ujao.
Hatua hiyo ina lengo la kuendeleza mchezo huo ambao ni wa pili kwa kupendwa nchii kwa mujibu wa
Mkuu wa Program wa Star Tv Dar es Salaam, Yusuph Kamote.
Kamote alisema kuwa kwa kupigia
kituo chao ambacho kina masafa marefu na kupatikana hadi maeneo ya
vijijini, mashabiki wa ngumi za kulipwa watapata fursa ya kujionea
‘live’ mapambano hayo tofauti na awali ambapo mashabiki wa ngumi za
kulipwa wa mjini walikuwa wanapata fursa hiyo.
“Tumezoa kuona mambo haya
katika soka lakini sasa Star Tv imepanua wigo na kuingia kwenye ngumi,
tutaonyesha live mapambano yote ambayo Hall of Fame itayaandaa iwe ya
hapa nchini au nje ya nchi,” alisema Kamote.
Ofisa Mtendaji mkuu wa Hall of
Fame, Jay Msangi alisema makubaliano hayo yanatoa fursa kwa kampuni,
taasisi na mashirika kujitokeza kudhamini ngumi na kujitangaza ndani na
nje ya nchi.
“Mpango uliopo ni kuandaa
mapambano sita ya kimataifa kila mwaka ambayo yatafanyika hapa nchini na
mengine nje ya nchi, hivyo katika kila pambano moja, Kampuni ya Star
Tv italitangaza kwa siku 35 na siku ya pambano litarushwa live, kama
litafanyika Dar es Salaam, watazamaji wa Star Tv wa mikoani watapata
fursa ya kulishuhudia vivyo hivyo na wale wa Dar es Salaam ambao
hawatakwenda ukumbini.
“Makubaliano haya sasa
yanafungua milango kwa kampuni, taasisi na nashirika kutumia nafasi hiyo
kudhamini masumbwi na kujitangaza kila siku katika siku 35 kila baada
ya miezi miwili.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni
inayowasimamia mabondia hapa nchini ya Respect Eagle, Chief Kiumbe
alisema makubaliano hayo yatasaidia kuinua mchezo wa ngumi na mabondia
hapa nchini.
“Tumekuwa tukishuhudia
mashabiki wakikesha kusubiri mapambano ya Ulaya, tunataka hamasa hiyo
ifanyije pia katika mapambano ya hapa nyumbani na tunaamini kwa umoja
huu tutafanikiwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni