Msajili
wa Hazina, Lawrence Mafuru akitoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo mbele ya
waandishi wa habari. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Cosmas
Kimario.
Alisema
kuwa rais aliagiza BoT kuzisimamia benki ambazo zimekuwa hazitoi faida
ili ziweze kusimama zenyewe na kuacha kutumia pesa ya umma ambayo
imekuwa haizalishi faida yoyote na hivyo kuonekana inafanya matumizi
mabaya ya fedha za serikali.
“Rais
alitaka hatua zichukuliwe ili kuzifanya benki hizo ikiwepo Twiga
kusimamiwa ili ziweze kuwa na tija na mwenyewe aliweka wazi kuwa hayupo
tayari pesa ya umma kutumiwa bila faida,
“Baada
ya hilo tumeanza kutafuta njia mbadala kuona ni jinsi gani itaweza
kufanya vizuri kama ikishindikana tutatafuta hata wawekezaji lakini
biashara itaendelea kuwepo kama kawaida,” alisema Mafuru.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kupata maelezo
kutoka kwa Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru kuhusu benki ya Twiga
Bancorp.
Kumekuwepo
na maneno mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu benki ya Twiga
Bancorp, tangu Rais John Magufuli alipoiagiza Benki Kuu ya Tanzania
(BoT) kuchukua hatua kwa benki zote ambazo zimekuwa hazifanya vizuri
ikiwepo benki ya Twiga na hivyo wananchi wengi wakawa wakiamini kuwa
benki hiyo itafutwa
Akielezea
kuhusu hatua zinazochukuliwa kwa benki hiyo, Msajili wa Hazina,
Lawrence Mafuru alisema kuwa ni kweli Rais Magufuli aliagiza jambo hilo
lakini alikuwa na maana nyingine tofauti na watu wengi ambavyo wamekuwa
wakizunguzia jambo hilo ambalo kwa namna kubwa anaamini linachangiwa na
vyombo vya habari.
Aidha
alieleza kuwa kumekuwepo na taarifa kuwa wateja wa benki hiyo wapo
katika hatari ya kupoteza pesa zao kutokana na benki hiyo kuwa katika
hasara na hivyo kuwatoa hofu kuwa benki ipo na pesa zipo salama na
wasiwe na wasiwasi kuhusu hilo.
Pia
Mafuru aliongeza kuwa pamoja na kuwa katika mpango wa kutafuta mbinu
mpya ya kutumia ili kuifanya benki hiyo kuwa na tija lakini pia taarifa
ambayo imetolewa wiki iliyopita inaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza benki
hiyo imeingiza faida na hivyo kuwa na matumaini mapya kuwa kuna
uwezekano wa benki hiyo kuanza kufanya vizuri katika biashara.
0 maoni:
Chapisha Maoni