……………………………..
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imesema lengo kuu la kufanywa tamasha la Utamaduni wa Mzanzibar ni
kuwaunganisha wazanzibar katika kulinda na kudumisha utamaduni huo.
Hayo yameelezwa mshauri wa Raisi
katika mambo ya utamaduni Chimbeni Kheri katika ufungaji wa tamasha la
21la utamaduni wa mzanzibar huko Fukuchani Wilaya ya kaskazini A”.
Amesema kuwa utamaduni huo pia
unawakutanisha wazanzibar kutoka sehemu mabali mbali ili waweze
kubadilishana mawazo juu ya njia bora ya kuendeleza utamaduni kupitia
njia ya sanaa.
Aidha amesema utamaduni ni roho ya
taifa hivyo unahitaji kuenziwa , kuendelezwa, kurithiwa na watoto wetu
katika michezo mbali mbali ya kiutamaduni .
“ Utamaduni ni muhimu sana kwani
hujenga afya ,kukuwa kwa kiakili na hupata ajira kwani dunia ya sasa
inazingatia sekta ya sanaa na utamaduni katika ustawi wa maendeleo ya
kimataifa.Alisema Chimbeni.
Hata hivyo ameeleza kuwa majanga
mengi katika jamii hujitokeza kwa kuacha mila na desturi za kizanzibar
hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuurejesha utamaduni wetu .
Sambamba na hayo amesema kuwa
Serikali imeweka mazingira mzuri yakuwawezesha Wasanii wa fani zote ili
kuweza kunufaika na kazi zao ili kuweza kuchangia pato la taifa .
“Katika suala la utamaduni
serikali imechukuwa hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na kuifanyia
marekebisho sheria inayohusu mambo ya utamaduni ili iendane na mahitaji
ya Jamii” Alisema mshauri huyo.
Nae Waziri waHabari Utalii
Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma amesema Wizara yake itashirikaana
na Wizara ya elimu kuhakikisha somo la utamaduni linarudi katika skuli
ili watoto waweze kuzijuwa mila na utamaduni wao .
Waziri huyo amefafanuwa zaidi kuwa
suala la utamaduni litaendelea kuwepo na kuwa la kihistoria na kila
mmoja anatakiwa kuwa balozi wa mwenziwe ili kuweza kuulinda utamaduni
huo usipotee katika visiwa vyetu.
Sambamba na hayo Tamasha hilo
limejumuisha michezo mbalimbali ya kiutamaduni ambapo kauli mbiu ya
mwaka huu ni Dumisha utamaduni na amani , piga vita udhalilishaji .
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
0 maoni:
Chapisha Maoni