Vijana wakipasha mara baada ya kufika kwenye viwanja vya Nyerere Squre.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson
akiongoza Mbio za Tulia Marathon KM 5 zilizofanyika leo asubuhi kuanzia
Bungeni Mpaka Nyerere Square zikishirikishwa wabunge mbalimbali wakuu wa
wilaya na vijana kama juhudi za kuunga mkono Juhudi za Rais John Pombe
Magufuli katika kuwaletea wananchi maendeleo nchini kushoto ni Anthony
Mtaka Rais wa Chama cha Riadha Nchini RT.
Baada ya mbio hizo walikwenda
kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha Watoto Yatima kiitwacho
kijiji cha Matumaini kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.Wakati wa
kutoa msaada huo Dkt Tulia alisema kuwa ni vvema kila Mkoa ukawa na
vikundi mbalimbali kikiwemo cha Wazalendo wakafanya shughuli za Kijamii
kusaidia makundi mbalimbali
0 maoni:
Chapisha Maoni