Seleman
Mgoto ambaye amepoteza uwezo wa kuona kabisa macho yake mawili baada ya
kutumia dawa hizo wakati akizungumza na waandishi kuhusina na
changamoto aliyonayo na kuomba msaada kwa wadau mbali mbali kuweza
kumsaidia.
Dada
wa Seleman Mgoto Luiza Mdachi wakati aliozungumza na waandishi
kuhusiana na matatizo aliyiyapata kaka yake ya kupoteza kabisa uwezo wa
kuona na jinsi familia yake ambayo ipo katika wakati mgumu.
(PICHA NA VICTOR MASANGU).
……………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI
MKAZI
mmoja ajulikanaye kwa jina la Seleman Mgoto (42)anayeishi katika
kitongoji cha Janga kilichopo eneo la Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoa wa
Pwani ameathirika macho yake mawili na kupoteza kabisa uwezo wa kuona
baada ya kutumia dawa ya kutibu malaria aina ya Fansider hivyo
anahitaji msaada wa kiasi cha shilingi milioni 18 kwa ajili ya kwenda
kupatiwa matibabu zaidi nchini India.
Hayo
yamebainika baada ya mwandishi habari hizi kuweza kufika nyumbani kwa
kaka yake maeneo ya mlandizi ambapo ndipo anapoishi kwa sasa baada ya
kupatwa na tatizo hilo na kuweza kuzungumza naye kuhusiana na mkasa wa
tukio hilo lililompata.
Akizunguza
kwa masikitiko makubwa Mgoto alisema kwamba mnano agosti 2012
alikuwa anaumwa na alipokwenda kupimwa aligundulika kuwa na wadudu
tisa wa ugonjwa wa malaria ndipo alipoandika dawa aina ya fansider na
kuamua kwenda kuzinunua katika moja la duka la madawa lililopo maeneo
hayo ya mlandizi na baada ya kuzimeza hali yake baada ya siku mbili
ilianza kubadilika kutokana na sumu kali iliyokuwepo mwilini mwake .
“Mimi
mwezi agosti mwaka 2012 ndugu zangu waandishi niliweza kuumwa na
nilipoenda kupima afya niligundulika nina malaria, na baada ya hapo
niliweza kuandikiwa dawa na nikaenda kununua dawa aina ya fansider, ila
baada ya siku mbii hali yangu iiweza kubadilika na nilipokwenda kituo
cha afya niilazwa kwa ajili matibabu zaidi,”alisema.
Aidha
akifafanua kuhusina na kuangaika katika hospitali mbali mbali kwa ajili
ya matibabu alisema kwamba mara ya mwisho alikwenda kuwaona madaktari
bingwa wa hospitari ya CCBRT ya jijini Dar es salaam ambapo walimwambia
macho yake kwa hapa Tanzania hayawezi kutibiwa mpaka aende nchini India
ndio yanaweza kupona.
Pia
katika hatua nyingine amesema kwamba kwa sasa maisha yake yamekuwa ni
magumu sana kutokana na kutokuwa na kipato chochote kile anachokiingiza
ukizingatia ana familia mke pamoja na watoto watatu ambao wanamtegemea
kwa kila kitu ambapo watoto wengine wawili wapo wanasoma sekondari
hivyo kunahitajika mahitaji mengine ya msingi.
Mwenyekiti
wa kamati maalumu ya kumsaidia kwenda kupatiwa matibabu nchini India
Eria Chaofu pamoja na Luiza Mdachi ambaye ni dada yake wamesema kwamba
familia imeangaika kwa hali na mali kwa kipindi cha miaka mitatu
katika hospitali mbali mbali kwa ajili ya kumtibia bila ya kupata
mafanikio yoyote kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha. miaka mitatu
Aidha
Mwenyekiti huyo amemwomba Rais wa awamu ya tano Dr.John Mgufuli
kumsaidia mgonjwa huyo pamoja na wadau wengine wakiwemo wakuu wa wilaya,
wabunge, wakuu wa miko pamoja na Wizara ya afya ili aweze kwenda
kutibiwa na kurudi katika hali.
Kwa
mtu yoyote ambaye ameguswa na anahitaji kumsaidia mchango wake kwa
hali na mali Seleman Mgoto ambaye amepoteza uwezo wa kuona kabisa wa
macho yake mawili,atume kwa tigo pesa –0655-413939 au M-PESA 0754-413939 na akaunti namba NMB -80110000915 kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu nchini India kwani zinahitajika shilingi milioni 18.
0 maoni:
Chapisha Maoni