Mbunge
wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (kulia), akizungumza Dar es Salaam
leo na wafanyakazi wa Kampuni ya M/S Yassa General Supplies Limited
iliyokodishwa kiwanja kilichopo nyuma ya Kituo cha Polisi Buguruni
ambapo ametoa siku tatu waondoke kupisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya
Buguruni. Mapato ya kiwanja hicho kwa zaidi ya miaka 10 yalikuwa
hayajulikani yalipokuwa yakienda.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Buguruni, Remmy Mishehe (kulia), akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusu kiwanja hicho.
Maelezo zaidi yakitolewa.
Mmoja
wa mtu aliyedaiwa ni dereva wa kampuni hiyo, akidhibitiwa baada ya
kudaiwa kutoa lugha ambayo siyo nzuri mbele ya mbunge wakati wa ziara ya
mbunge huyo kukagua kiwanja hicho.
Malori ya kampuni hiyo yakiwa yameegeshwa kwenye kiwanja hicho.
Mmoja
wa viongozi wa kampuni hiyo akitoa maelezo kwa Mbunge Bonnah Kaluwa
(kushoto). Katikati mwenye suti ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya
Kata ya Buguruni, Barua Mwakilanga.
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE
wa Jimbo la Segerea Bonnah Kaluwa amefanikiwa kukirejesha kiwanja kwa
wananchi wa Kata ya Buguruni kilichokuwa kikitumika kuegesha magari kwa
malipo bila kujulikana matumizi ya fedha hizo.
Kiwanja
hicho ambacho kipo nyuma ya kituo cha Polisi Buguruni kilikuwa
kimetengwa miaka mingi iliyopita kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya
Sekondari ya Buguruni.
Akizungumza
wakati akikagua kiwanja hicho Dar es Salaam leo asubuhi ambacho
kinatumiwa na Kampuni ya M/S Yassa General Supplies Limited kuegesha
magari yao alisema wametoa siku tatu wawe wameondoka ili waanze mara
moja ujenzi wa shule hiyo ambapo jumla ya sh. milioni 40 za kuanzia
ujenzi huo zimetengwa.
"Kata
ya Buguruni haina shule hata moja ya Sekondari kupatikana kwa kiwanja
hiki kitasaidia watoto kupata shule katika kata yao badala ya kwenda
shule zingine za mbali" alisema Kaluwa.
Kaluwa
aliongeza kuwa waliokuwa wakitumia kiwanja hicho waliingia mkataba na
uongozi wa Kata ya Buguruni ambapo katika kipengere namba nne kilieleza
kuwa ikifika wakati eneo hilo likihitajika basi mpangaji atalazimika
kuondoka.
"Kwa
kuwa mpangaji wa eneo hilo yupo na mkataba unajieleza wenyewe kupitia
kipengere hicho tunaomba wahusika watupishe haraka iwezekanavyo tuanze
ujenzi wa sekondari" alisema Kaluwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni