Postedy by Esta Malibiche on july 18
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Action Mart Bwana Alex Msama akionyesha Stika za
TRA zinazodaiwa kutolewa kimyemela na Baadhi ya watumishi wa TRA wasio
waaminifu kwa kushirikiana na watu wanaodurufu kazi za wasanii kinyemela
ili kujipatia kipato.
Kutokana
na hali hiyo Msama Amempongeza Waziri wa Habari , Uramaduni, Sanaa na
Michezo Mh. Nape Nnauye kwa kazi aliyoifanya kutoka ofisini na kuenda
kwenye maduka mbalimbali Kariakoo kwa ajili ya kusaka wezi wa kazi feki
za wasanii.
Amesema
Jambo hilo limemtia moyo kama mpigania haki wa kazi za wasanii ambaye
amekuwa akipambana kila siku ili wasanii waweze kufaidika na jasho lao
na ataendelea na kazi ya kuhakikisha wezi wote wa kazi za sanaa
wanashughulikiwa kisheria na kuwafanya wasanii nao wanafaidi jasho lao.
Bwana Alex Msama akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Bwana
Alex Msama akionyesha baadhi ya stika za TRA zinazodaiwa kuibiwa na
kugawiwa kinyemela kwa wauzaji wa Kazi feki za wasanii.
Hii ni moja ya CD feki iliyobandikwa stika za TRA.
Bwana Alex Msama akionyesha CD Feki na Stika zinazodaiwa kutuolewa kinyemela na baadhi ya watumishi wa wasio waaminifu.
0 maoni:
Chapisha Maoni