Dua
na sala za Watanzania zielekezwe pia kwa timu ya Taifa ya Mpira wa
Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’,
iliyoondoka mapema jana saa 12.00 Uwanja wa Ndege ya Mwalimu Julius K.
Nyerere, Dar es Salaam, Tanzania kwenda Antananarivo, Madagascar kupitia
Uwanja wa Ndege wa Ndege ya Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika
Kusini.
Serengeti
Boys inayokwenda kuweka kambi huko Antananarivo, Madagascar inatarajiwa
kufika huko saa 8.10 mchana. Timu hiyo inajiandaa kucheza na Afrika
Kusini katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.
Mchezo
wa marudiano utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam,
ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Serengeti
ipo kwenye ushindani wa kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani huko Madagascar.
Wakati
mkuu wa msafara akiwa ni Ayoub Shaibu Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Soka la Vijana, maofisa wengine waliosafiri na timu hiyo ni
Kocha Mkuu, Bakari Nyundo Shime, Daktari wa timu hiyo, Shecky Francis
Mngazija na Mtunza Vifaa, Andrew Vanance Andrew pamoja na Juma Kaseja
Juma ambaye kwa muda amechukua nafasi ya makocha wasaidizi, Sebastian
Nkoma na Muharam Mohammed ‘Shilton’ wanaohudhuria kozi ya makocha ngazi
ya juu inayoratibiwa na CAF.
Nyota
waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, Kelvin
Deogratius Kayego na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana
Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson
Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick Vitalis
Nkosi.
Viungo
ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali,
Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi Ada
huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar
Mkomola na Muhsin Malima Makame.
“Najua
mchezo utakuwa mgumu, lakini nakiamini kikosi change. Kiko imara,”
amesema Shime, maarufu zaidi kwa jina la Mchawi Mweusi.
Serengeti
Boys inakwenda kucheza na Afrika Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli kwa
jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa. Mshindi wa
jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika Kusini, atacheza na timu mshindi
kati ya Namibia na Congo-Brazaville.
Hivi
karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki
mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF
International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya
kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
0 maoni:
Chapisha Maoni